Header Ads Widget

UJENZI KITUO CHA AFYA MLOWO MBOZI CHAZINDULIWA.

Katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wananchi wa Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi mkoani Songwe, wamepata sababu ya kutabasamu baada ya  kufanyika kwa uzinduzi wa ujenzi mradi wa kituo cha afya hitaji lililosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi hao.

Hafla ya maadhimisho hayo imeongozwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, Mhe Hamad Mbega ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi kama ishara ya kuhamasisha wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye maendeleo katika Mkoa huo.

Akizungumza katika  maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Mbega amesema ujenzi wa kituo hicho utasaidia wananchi kuwaondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika Hospitalii ya Wilaya na mkoa zilizoko mjini Vwawa.


"Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea Shilingi million 623 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki cha afya (Mlowo) ambapo wananchi walikiwa wakifuata huduma hii mbali na kilikuwa ni kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Mlowo", amesema Mhe. Mbega.


"Rasmi tumezindua ujenzi huu ambapo  kitapunguza adha waliyokuwa wakikutana nayo wananchi wa Kata hii (Mlowo) na mradi huu ni hatua kubwa ya kuboresha huduma kwa wakazi wa Mlowo na vijiji jirani" ameongeza kiongozi huyo.


Kupitia mpango wa uboreshaji wa huduma za afya, eneo la Mlowo ilioorodhezeshwa kuwa miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na mradi wa maendeleo wa afya.

Mhe. Mbega amesema kuwa tathmini ilionesha kuwa Mlowo ni eneo lenye idadi kubwa ya  watu ambapo inawakazi zaidi ya elfu 66 yenye vitongoji 24 ambapo uhitaji wa huduma za afya ulikuwa ni mkubwa

"Kwa muda wa miaka kadhaa wakazi wa Mlowo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za  afya hali hali iliyokuwa ikiwalazimu kusafiri umbali mrefu",ameeleza Mkuu huyo wa wilaya ya Mbozi akihitimisha hotuba yake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI