Header Ads Widget

SHILINGI BILIONI 73.6 KUKAMILISHA MRADI WA HEET SUAp

 

Na Lilian Kasenene, Morogoro 

Matukio DaimaApp 


Zaidi ya Sh Bil 73.6 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya majengo pamoja na ujenzi wa majengo mapya kwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa Kampasi zake zote hapa nchini kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Majenzi ya Kiuchumi (HEET).


Mtaalamu wa Majenzi Mradi wa HEET kutoka SUA Mhandisi Japhet Maduhu alisema hayo wakati wa kukagua mwenendo wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya

mradi huo unatekelezwa katika Kampasi tatu, Kampasi ya Mizengo Pinda iliyopo Katavi, Solomoni Mahlangu Mazimbu –Morogoro na Kampasi Kuu ya Morogoro.


Mhandisi Maduhu alisema nia ni kufanikisha dhima ya kufufua na kupanua uwezo wa vyuo vikuu hivyo katika maendeleo ya kiuchumi na umuhimu wa soko la ajira.

Alisema mradi unahusisha majengo mapya tisa yakiwemo majengo 03 ya maabara, hosteli 02 na Majengo mengine 04 kwa ajili ya shughuli za kitaaluma, huku ukarabati ukihusisha majengo 18 ambayo ujenzi wake umelenga kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ili kuweza kukidhi kwa wenye mahitaji maalumu kufuatia miundombinu ya majengo hayo kuwa na mifumo ya kizamani ambapo sasa yatawekewa mifumo mipya ya TEHAMA na umeme

“Kwa ujumla mradi umefikia asilimia 8 ya ujenzi wake, wakandarasi wote wapo wanaendelelea na kazi, Mradi wa HEET kwa Chuo chetu umeweza kutupatia Zaidi ya shilingi 73.6 ambapo katika fedha hizo Zaidi ya shilingi bilioni 58 zimetengwa kusimamia majenzi kwa kpampasi zote,”alisema Mhandisi Maduhu


Alisema ukarabati wa mejngo unatekelekezwa kwa kipindi cha Mwaka mmoja, umeanza kutekelezwa Mwezi Disemba Mwaka 2024, unatazamiwa kukoma Disemba Mwaka huu, huku ujenzi wa majengo mapya ukitekelezwa kwa miezi 18 utahitimishwa Mwezi Juni 2026.


Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi Kampasi ya Solomoni Mahlangu Mhandisi Enock Kamagu alisema ujenzi unaendelea vizuri kwasasa kwa kampasi hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto ya mvua zinazoendelea kunyesha kwasasa mkoani Morogoro.


Alisema awali Mkandarasi alikabiliwa na changamoto ya kuchelewesha vifaa eneo la mradi lakini sasa wanaimani kwa mwenendo wa mkandarasi huyo atakamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa.


Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano na Masoko SUA Suzana Magobeko alisema kukamilika kwa mradi huo unatazamiwa kuchagiza ongezeko la udahili wa wanafunzi kwa Kampasi zote tatu za Chuo hicho pamoja na kukuza wigo wa kuifikia jamii kwa ukubwa hasa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


Alisema ujenzi na ukarabati wa  miundombinu inayohitajika kwa ufundishji na utafiti mzuri na kwa mafunzo ya kiwango cha juu zaidi, unawagusa walimu, watafiti, wasimamizi wanaohitajika na vyuo vikuu ili kufikia uwezo wao kamili.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI