Header Ads Widget

RC MTAMBI AKABIDHI MADAWATI 600 AVUTIWA NA UTENDAJI WA MBUNGE MATHAYO



Na Shomari Binda-Musoma 

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amemuita mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kama mbunge anayechapa kazi mkoa wa Mara.


Kutokana na uchapa kazi huo amemuita kuwa  ni jembe anayestahili kulipwa kwa wema wake anaowatendea wananchi wa jimbo la Musoma mjini.


Kauli hiyo ameitoa leo aprili 30,2025 alipokuwa akikabidhiwa madawati,viti na meza 600 vilivyotengenezwa na mbunge huyo pamoja na wadau wa elimu kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.


Amesema mbunge Mathayo ni mmoja wa wabunge wanaofanya vizuri katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yakiwemo ya elimu.


Mtambi amesema madawati,meza pamoja na viti 300 awamu ya kwanza vilivyotengenezwa na mbunge huyo kwa kutumia kiasi cha zaidi ya milioni 28 anastahili kulipwa kwa wema huo.


" Huyu mbunge anatenda wema kwa kweli sitaki kuingia huko sana msije kusema namaanisha kitu lakini anastahili kulipwa kwa wema.


" Madawati viti na meza hizi zinakwenda kuwasaidia watoto wetu mashuleni kusoma huku wàkiwa wamekaa sehemu nzuri",amesema.


Mkuu huyo amesema ameanzisha kampeni ya mtoto wa shule za mkoa wa Mara kutokukaa chini na kuhakikisha chakula shuleni linakuwa suala la lazima.


Aidha ameishukuru benki ya Azania pamoja na taasisi ya Nyansaho Foundation kwa kuchangia madawati,viti pamoja na meza nyingine 300.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha kibali kinapatikana cha kuvuna miti ya mbao na kupatikana madawati pamoja na viti na meza.

Mathayo amesema hii ni awamu ya kwanza ya madawati,viti na meza hizo na yataendelea kutengenezwa kwa awamu nyingine ili kuhakikisha hakuna mtoto anayejaa chini jimbo la Musoma mjini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI