Sehemu ya pili..
Makala iliyopita tumeona changamoto alizopitia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Hamis A. Kigwangalla na namna alivyokuja na maono ya kuwakomboa watu maskini (wananchi) kijamii na kiuchumi.
Lakini pia tuliona jinsi dhamira hiyo ilivyoishia njiani baada ya kukutana na vikwazo vingi alivyowekewa na bwana Bashe kupitia viongozi aliowatumia wa chama na serikali kiasi cha viongozi hao kumbagua na kumchukia.
Sote tunajua kwamba kila binadamu ana hulka ya kukasirika lakini si wote tunaojua kwamba si kila binadamu humkasirikia mtu sahihi, kwa kiwango sahihi, kwa muda sahihi, na kwa sababu sahihi.
Hilo si rahisi, lakini linawezekana kwa watu maalumu.
Dk. Kigwangalla alichukiwa kikweli na viongozi hao kutokana na sababu zao binafsi hasa walizomezeshwa na bwana Bashe.
Dk. Kigwangalla yeye hakutaka wananchi wazidi kuendelea kukaa katika hali ambazo hazifai (yaani hakutaka wananchi waendelee kulaghaiwa kwa kuaminishwa yale maisha duni na ya hovyo hovyo kuwa ndiyo ya maana, kuwa omba omba, kunyanyaswa na kugeuzwa madaraja ya watu wachache kujinufaisha binafsi).
Yeye alitamka hadharani tena kwenye mkutano wa wananchi kuwa, "Mimi siwezi kumsaidia mtu mmoja mmoja", kauli hii iliwakwaza baadhi ya watu hasa viongozi ndani ya CCM ambao ni wavivu wa kufikiri.
Lakini kauli hii ilipokewa vema kwa upande wa watu makini, wapo walioilinganisha kauli hiyo kuwa ni mfumo wa malezi ya Bata, tofauti na malezi ya Kuku, kwamba, Bata yeye huwalea watoto wake katika mazingira ya kunitegemea kimaisha or kifikra, wakati kuku huwalea watoto wake katika mazingira tegemezi 'omba omba'.
Hivyo ndivyo tulivyojua kwamba, Dk. Kigwangalla hataki jamii ya watu omba omba kwa sababu jamii ya namna hiyo inakuwa nyuma kimaendeleo siku zote.
Kauli hiyo mbele ya umma ililenga kuwaandaa wananchi kisaikolojia, na siyo kwamba Kigwangalla hakupenda kusaidia watu wenye uhitaji, tunajua amesaidia watu wengi sana na ushahidi tunao.
Kwa nini Jimbo la Nzega liligawanywa mara mbili na kuzaa majimbo mawili ya Nzega Vijijini na Nzega Mjini?
Ni swali ambalo wengi walijiuliza mpaka sasa hawaelewi kiundani, ukweli ni kwamba Jimbo la Nzega liligawanywa kutokana na msukumo wa Bashe kwani wakati huo kulikuwa na msuguano mkubwa baina yake na Dk. Kigwangalla, walifikia hatua hata ya kutoleana Bastora.
Kutokana na kukubalika kwa Dk. Kigwangalla kwa wananchi, ilionekana kabisa kwamba endepo Jimbo halitagawanywa basi Bashe asingeweza kushinda uchaguzi wa 2015 na vita ingekuwa kali zaidi.
Mtu pekee aliyetumika ndani ya CCM na kumsaidia Bashe kupata Jimbo ni Katibu Mkuu wa CCM Kinana.
Wakati huo Kigwangalla alikuwa hashikiki kutokana na wananchi walivyomkubali, enzi hizo kama uliwahi kusikia majina yenye ufalme kama "Shimba Ng'osha" yaani Simba dume, "Chief Makaranga Ng'wanamwashi" na mengine yenye nasaba na ukombozi kama ya akina Fidel Castro wa Cuba na wakomunisti wengine duniani, basi alikuwa mbunge wa Nzega Dk. Kigwangalla.
*Dk. Kigwangalla ndani ya Jimbo jipya la Nzega Vijijini.*
Hapa kuna sura mbili zinazojitokeza katika uongozi wa Dk Hamis Kigwangalla baada ya kuwa katika Jimbo jipya la Nzega Vijijini, ambazo nitaelezea mojawapo hapa kwa ufupi na nyingine katika makala ijayo.
Sura hii ya kwanza ya uongozi wa Dk Kigwangalla hasa baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akitokea kwenye unaibu waziri wa Afya, Dk. alionekana kama kiongozi anayeendana na hulka ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, na hili alilitaja Rais mwenyewe akiwajumuisha pia akina Luhaga Mpina wakati na baada ya kuwateua kuwa mawaziri.
Japo alitumia lugha ngumu sana kwamba amewateua wasaidizi wake kwa vigezo na hulka zao za "ukichaa" (yaani watu wasiweza kuvumilia upumbavu na wapumbavu, ufisadi na uonevu) zinazoendana na hulka yeke.
Kauli ile ya Rais Magufuli ni kama aliongeza petroli kwenye moto, lakini hakujua pia kuwa aliwaongezea uadui mkubwa kwa mafisadi na wapumbavu.
Baada ya kupewa majukumu ya kitaifa, ilipelekea kuadimika ndani ya jimbo lake kutokana na majukumu ya kiserikali, basi mwenzake Bashe akautumia mwanya huo kumharibia kwa wananchi na kwa Rais pia.
Kwanza alijifanya kuwasaidia viongozi wa chama na baadhi ya wananchi wa jimboni kwa Kigwangalla na kuchochea chuki ya kumwoneaha mbunge wao hajali viongozi na wananchi wa jimbo lake.
Hata wakati wa ziara za viongozi wa chama na serikali ngazi ya mkoa na kitaifa, Bashe aliwatumia viongozi wa jimbo hilo kuwashawishi wananchi kuonesha hawamkubali mbunge wao Dk. Kigwangalla sipokuwa Bashe.
Kwa upande wa Rais, Bashe alitumia vyombo vya habari na wapinzani na wanaharakati kumchafua Kigwangalla, akamtumia hadi aliyekuwa katibu wa wizara ya maliasili ambaye sasa ni waziri wa elimu, Mkenda, Ndugai, Katibu Mkuu Bashiru na hata Makamu Samia.
Mipango yote hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na ikapelekea Dk. Kigwangalla kushuka kisiasa na taswira yake. Wengi wanakumbuka Rais Magufuli alitoa kauli kwa kile kilichoitwa "mgogoro wa Waziri wa maliasili, Dk Kigwangalla na katibu wake Mkenda" na kuwaagiza wapatane mara moja.
Pili, kilichoitwa "sakata la Dk. Kigwangalla na Mo Dewj", kwenye ishu hiyo alitumika katibu wa chama Bashiru ambaye naye aliongea kama kasuku, akakemea 'vikali' tena hadharani akimuunganisha na Nape.
Yote haya yaliibuliwa na hasimu wake bwana Bashe kupitia watu hao aliowatumia kumshugulikia Dk. Kigwangalla.
Kutokana na mbinu mbalimbali anazozitumia Bashe mpaka sasa kumhujumu Dk. Kigwangalla, amekuwa akifanya hivyo hata Jimbo la Bukene na ndiyomaana hasa imepelekea majimbo hayo kuonekana kuwa na ushindani mkubwa kutokana na wagombea kuwa wengi.
Hata wale wanasiasa waliotakiwa kugombea jimbo la Nzega Mjini amekuwa wakikimbilia majimbo haya hasa la Nzega Vijijini, wengine hawaendi kwa kuoenda bali kutokana na vitisho wanapotaka kugombea jimbo la Nzega Mjini.
Makala iliyopita nilisema kwamba Dk. Kigwangalla ni binadamu kama wengine na hivyo naye anayo mapungufu kama binadamu, nimeyaeleza haya katika sura hii ya kwanza lakini nitayaeleza zaidi katika makala ijayo ya tatu.
Kwiyeya Singu. 0784977072
0 Comments