Header Ads Widget

MKUCHIKA ATOA POLE KIFO CHA DIWANI KAKONKO, ALAANI MAUAJI

 

WAZIRI wa nchii ofisi ya Rais Ikulu George Mkuchika  (kulia) akimpa pole Mke wa Aliyekuwa Diwani wa kata ya Kiziguzigu wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambaye aliuawa April 3 mwaka huu kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana

Na Fadhili Abdallah, Habari na Matukio App Kigoma

WAZIRI wa nchii ofisi ya Rais Ikulu George Mkuchika amefika nyumbani kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Kiziguzigu wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kutoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu huku akikemea mauaji na kutaka watuhumiwa wasakwe na kuchukuliwa hatua kali.

Mkuchika alifika nyumbani kwa Marehemu Mpemba akiwa kwenye ziara ya kiserikali ya siku moja wilayani humo ambapo alisema kuwa haikubaliki kwa namna yeyote mtu mmoja au kikundi cha watu kusababisha mauaji kama hatua ya kulipiza kisasi badala ya kufuata taratibu za kisheria.

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza nyumbani kwa Diwani wa kata ya Kiziguzigu wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo WAZIRI wa nchii ofisi ya Rais Ikulu George Mkuchika alifika kutoa pole kwa familia ya marehemu

Akiwa msibani hapo Waziri huyo aliwasilisha salam za rambirambi za serikali na kusema kuwa viongozi wote wa serikali akiwemo Raisi Samia wameguswa na msiba huo na ndiyo sababu ya kuahirisha shughuli nyingine za ziara katika wilaya hiyo ili kufika msibani hapo na kutoa pole.



Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Jamal Tamim akizungumza nyumbani kwa Marehemu Martin Mpemba aliyekuwa Diwani wa kata ya Kiziguzigu wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo WAZIRI wa nchii ofisi ya Rais Ikulu George Mkuchika alifika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu

Akizungumza wakati wa safari hiyo ya Waziri Mkuchika kutoa pole kwenye msiba wa Diwani Mpemba, Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamal Tamim alisema kuwa chama kimepata pigo kwa kuondokewa na diwani huyo ambaye alikuwa na msimamo katika kupigia kelele kuomba miradi kwa ajili ya wananchi wake.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye alisema kuwa kama serikali kupitia polisi na vyombo vya ulinzi na usalama wameshaanza kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo kwa upelelezi mkali kuhakikisha wahusika wote wa tukio hilo wanakamatwa

Akitoa salam za familia pamoja na kupokea rambirambi Mtoto wa marehemu, Adam Martin Mpemba alisema kuwa wameshtushwa na kifo cha baba yako lakini anaamini kuwa serikali itachukua hatua kuwatafuta wahusika na hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI