Header Ads Widget

MJUMBE WA KAMATI KUU YA MICHEZO YA MEI MOSI TAIFA COMRADE JAPHARI MTORO AWASHUKURU WADAU WA MICHEZO SINGIDA

 

Comrade Japhari Mtoro

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Michezo ya Mei Mosi  Taifa Comrade Japhari Mtoro amewashukuru viongozi na wadau wa michezo mkoani Singida kwa namna walivyoshiriki kufanikisha mashindano hayo yaliyofanyika mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati ya fainali ya mpira wa miguu kati ya Tanesco na Hazina BW. Japhari alisema

"Mkoa wa Singida umeyapokea na kuyathamini sana mashindano ya michezo ya MEI MOSI Taifa. Tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, wadau mbalimbali wa Michezo pamoja na wananchi wote wa Singida.

Tumefurahia kucheza katika viwanja vizuri vya hadhi ya juu kabisa kama  Liti, Airtel kwa upande wa mpira wa miguu, Veta na Mwenge kwa mpira wa Netiboli na Mwaja kwa mpira wa Kikapu.

Aidha, tumefurahia kucheza katika hali ya hewa nzuri ya Singida iliyotuwezesha kupanga ratiba zetu siku nzima bila kikwazo chochote"

Vile vile Bw. Japhari amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kujali afya za wafanyakazi na kuhakikisha usalama wao katika kipindi chote cha michezo.

"Tunamshukuru na kumpongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kulinda afya na usalama wa wafanyakazi. Hii ni mara ya kwanza katika mashindano tunapewa Ambulance na madaktari wa Mkoa katika kila kiwanja cha michezo ukiacha madaktari wa timu.

Mashindano ya MEI MOSI Taifa yamehitimishwa tarehe 29 April, 2025 na yalianza tarehe 14 April, 2025 mkoani Singida.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI