Na Matukio Daima Media
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Iringa, Dr. Ritta Kabati amekabidhi baiskeli kwa mtoto mwenye ulemavu kutoka kata ya Image, Wilaya ya Kilolo anayefahamika kwa jina la Oliver Msumule.
Kabati ametoa baiskeli hiyo wakati wa Ibada ya Pasaka katika kanisa Katoliki parokia ya Myombwe iliyopo Image, wilayani Kilolo.
Amesema ameamua kukabidhi baiskeli hiyo kwa Oliver anayesoma darasa la Nne ili apate urahisi wa kwenda shule.
Pamoja na baiskeli hiyo, Kabati amempatia mguu utakaomsaidia katika shughuli zake.
Aidha, Kabati ameahidi kumsaidia mtoto huyo kusoma kwenye shule za bweni.
Kwa upande wake baba wa mtoto huyo, Zakayo Msumule amemshukuru Mbunge Ritta Kabati kwa kumkabidhi baiskeli na Mguu wa bandia mtoto wake ili kumuwezesha kuendelea na masoko.
Amesema awali ilikuwa ngumu kwa Oliver kwenda shule katika nyakati tofauti kutokana na kupata maumivu ya mguu ya kutembea umbali mrefu.
0 Comments