Na Shomari Binda-Matukio Daima-Butiama
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amssema ataendelea kuusemea mkoa wa Mara na kuomba fedha serikalini kwaajili ya utekelezaji wa miradi.
Kauli hiyo ameitoa leo aprili 21,2025 Kata ya Bwiregi wilayani Butiama alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa ilani ya mwaka 2020/2025 kwenye Kata hiyo.
Amesema katika kipindi cha utekelezaji wa ilanj ya kipindi hicho Kata hiyo imepokea zaidi ya bilioni 2 ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali.
Ghati amesema miradi iliyotekelezwa ni pamoja ya elimu,afya,maji na miundomninu ikiwa kufungua barabara.
Mbunge huyo amesema kamwe hawezi kuwa bubu kwa kuongea kwaajili ya mkoa wa Mara katika utekelezaji wa miradi.
Amesema licha ya kuongea kwa kipindi alichokaa bungeni amejua njia za kupita kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi.
" Nduhu zangu wana Bwiregi tuendelea kuishukuru serikali chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavuotupatia fedha mkoa wa Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
" Kwenye hii Kata yetu tumepokea fedha nyingi kutoka kwa Mama Samia na imetekeleza miradi na shukrani ya kumpa ni kumchagua kwa kura nyingi kwenye uchaguzi wa mwaka huu"amesema.
Kwa upande wake diwani wa Kata ya Bwiregi ameishukuru serikali kwa namna inavyowagusa wananchi kwa utekelezaji wa miradi.
Amesema wataendelea kumsemea vizuri Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan na kumuahidi kumpa kura za kishindo muda ukifika.
0 Comments