Header Ads Widget

CRDB BANK YA KWANZA KUTHIBITISHA USHIRIKI BONANZA LA MUUNGANO MUSOMA

 


Na Matukio Daima Media-Musoma 

TIMU ya watumishi wa benki ya CRDB tawi la Musoma imekuwa ya kwanza kuthibitisha ushiriki wa bonanza la Muungano Bankers bonanza aprili 26 2025.

Bonanza hilo lenye lengo la kusherehekea sikukuu ya Muungano na kujenga mahusiano limepangwa kufanyika siku ya sherehe za Muungano.

Mratibu wa bonanza hilo Shomari Binda amesema kila wakati wa sherehe za Muungano limekuwa likiandaliwa bonanza kwa kushirikisha maeneo tofauti na kwa mwaka huu wamewafikia watumishi wa taasisi za fedha waliopo Musoma.

Amesema wamezifikisha taarifa taasisi hizo na benki ya CRDB wamekuwa wa kwanza kuthibitisha ushiriki wao mara baada ya kupata taarifa hiyo.

Meneja wa benki hiyo tawi la Musoma Jerome Mwenda amesema anatambua umuhimu wa michezo kwaajili ya afya na kuweka mwili vizuri hivyo wapo tayari kushiriki.

Amesema kama meneja yupo tayari kuingiza timu kwenye bonanza hilo na kazi anawaachia viongozi wa timu kujiandaa na kuingiza timu uwanjani.

" Sisi tupo tayari tunajua mabonanza licha ya kuweka afya vizuri lakini pia tunajenga mahusiano na wenzetu tunaokutana nao hivyo tupo tayari kushiriki siku hiyo.

" Tunaposherekea Muungano wetu yapo matukio mbalimbali na hili sisi tupo tunawaomba wenzetu pia waje tukutane uwanjani lakini pia tutabadilishana mawazo siku hiyo",amesema

Wengine waliofikishiwa ujumbe wa ushiriki wa bonanza la Muungano ni NBC benki,TCB benki,NMB benki,Finca benki pamoja na NSSF.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI