Header Ads Widget

MAHAKAMA YA JUU YA UGANDA YAMNYIMA DHAMANA BESIGYE NA LUTALE


 Besigye alipokelewa na wafuasi wake baada ya kufika mahakamani tarehe 20 Novemba

Mahakama ya juu ya Kampala imemnyima dhamana kiongozi wa upinzani Besigye na mwenzake Hajj Lutale wakitaja kuwa kesi inayowakabili ni nzito na kutokana na ushawishi wao huenda wakaingilia kati uchunguzi.

Ni siku ya 147 tangu wawili hao kuzuiliwa baada ya kukamatwa mjini Nairobi mwezi Novemba mwaka jana.

Kulingana na mahakama hiyo dhamana iliyowasilishwa na Kisza Besigye na Hajj Lutale ni dhabiti na kusema kuwa waliafiki viwango hitajika vya kupewa dhamana.

Hata hivyo Jaji aliyekuwa akisimamia kesi hiyo alidinda kuwapa dhamana akieleza kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Mgombea wa mara nne wa urais nchini Kenya pamoja na msaidizi wake wanakabiliwa na shtaka la uhaini ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Kulingana na upande wa mashtaka Besigye,kapteni Denis Oola na wengine ambao hawajakamatwa wanadaiwa walifanya jaribio la mapinduzi kati ya mwaka 2023 na mwezi Novemba 2024.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI