Header Ads Widget

MAHAKAMA KUU YA KAKAMEGA KENYA YAONDOA MARUFUKU KWA KIPA PATRICK MATASI


Patrick Matasi alicheza mechi yake ya kimataifa mwaka wa 2017 lakini hajaichezea Kenya tangu mwaka jana

 Mahakama Kuu ya Kakamega imeondoa marufuku dhidi ya mlinda lango wa timu ya Taifa ya Soka ya Kenya Harambee stars na klabu ya Kakamega Homeboys Patrick Matasi iliyowekwa na shirikisho la soka nchini (FKF)kufuatia madai ya kuhusika katika upangaji wa matokeo ya mechi za soka.

Mahakama hiyo siku ya Jumane ilimpa ruhusa Matasi kurejea katika shuhul zake zote za soka zinazoambatana na shirikisho la FKF hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa na kukamilika.

Mwezi Machi mwaka huu, Patrick Matasi alipigwa marufuku ya siku 90 na FKF baada ya video moja kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha akihusika katika kile kinachoonekana kupanga matokeo ya mechi na mtu asiyejulikana.

Kwa mujibu wa hukumu ya Jaji SN Mbungi, mshtakiwa hajajibu shtaka hili wala hakuhudhuria kesi.

Shtaka hili halijapingwa wala kukubaliwa,kwa hivyo natoa amri ya kihafidhina ya kumzuiya yoyote kumpiga marufuku mshtakiwa kuendelea na shughuli zake za soka.

Aidha jaji huyo alisema mlalamishi anapaswa kuwasilisha shtaka hili rasmi dhidi ya mshtakiwa ambaye ataruhusiwa kukubali ama kukataa mashtaka ndani ya siku 30 zijazo kuanzia leo (Jumanne, Machi 8).

Hii si mara ya kwanza kwa visa vya wachezaji soka nchini Kenya kuhusishwa katika madai ya kushirikiana na watu wasiojulikana katika jambo la upangaji wa matokeo ya mechi.Patrcik Matasi anaichezea klabu ya Kakamega Homeboyz inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Kenya na pia ameiwakilisha timu ya taifa ya soka Harambee stars mechi 30.

Mahakama hiyo aidha imelipatia shirikisho la soka nchini FKF siku 30 kujibu agizo hilo..

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 4 Mwezi Juni mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI