Header Ads Widget

CHINA YATOA WITO KWA DUNIA KUUNGANA DHIDI YA 'UDHALIMU WA KIBIASHARA' WA TRUMP

 



China imetoa wito kwa ulimwengu kuungana dhidi ya ushuru wa Trump huku wauzaji bidhaa nje wa nchi hiyo wakikabiliwa na ushuru mpya wa Marekani ambao umepanda hadi 104%.

"Umoja wa kimataifa unaweza kushinda udhalimu wa kibiashara," ilisema tahariri katika gazeti la serikali la China Daily, ikibainisha ushirikiano wa Beijing na Japan, Korea Kusini na uchumi mwingine wa Asia. Makala nyingine ilitaka Umoja wa Ulaya kufanya kazi nao "kuendeleza biashara huria na ushirikiano wa pande nyingi".

Beijing "inapinga na haitakubali kamwe vitendo hivyo vya kikatili na uonevu," msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lin Jian aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

Ushuru huo umetangazwa wakati mgumu kwa uchumi wa China uliodorora: matumizi ya ndani yanasalia kuwa chini na mauzo ya nje bado ni kichocheo kikuu cha ukuaji.

Asili kubwa ya ushuru wa Trump pia imewaacha wafanyabiashara wa China wakihangaika kufanya marekebisho katika usambazaji - huku nchi nyingi zikiathiriwa, kampuni zinasema ni vigumu kupata njia katika hali hii ya kutokuwa na uhakika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI