Header Ads Widget

MADIWANI MJI NJOMBE WATAKA KUONGEZWA NGUVU UDHIBITI WA MAPATO.

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Licha ya Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe kufikia Asilimia 87 ya makusanyo ya mapato ya ndani Hadi mwezi Machi Mwaka huu Madiwani wametaka kuongezwa kwa nguvu ya udhibiti wa mapato haswa maeneo ya vijijini ambapo Kuna uzalishaji mkubwa wa mazao ya Kilimo na misitu. 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete


Katika kikao cha Baraza la madiwani Cha robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha wa 2024/2025 Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema Hadi sasa bilioni 33.9 zimekusanywa kuanzia mwezi januari Hadi Machi  huku mapato ya ndani wakikusanya shilingi bilioni 5.97 sawa na Asilimia 87.


Baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo akiwemo Edwin Mwanzinga,Yurick Msemwa na Anjela Mwangeni  wametaka kudhibitiwa kwa mianya ya mapato pamoja na kuhakikisha mitambo ya ujenzi inaingiza mapato ili kuongeza kiwango Cha makusanyo.


Wamesema wataalamu wanapaswa kusaidia Halmashauri iweze kukusanya Fedha Zaidi kwani Kuna baadhi ya Mapato yanatoroshwa na kuikosesha Halmashauri Fedha.



"Napongeza kazi inayofanyika kwenye mapato,tunatakiwa kufahamu tuna misimu miwili ya ukusanyaji,nguvu kubwa tuelekeze kwenye peak season ambapo kuna uzalishaji mkubwa na ukusanyaji pia huwa mkubwa,tukiendelea kudhibiti  tutapata mapato mengi sana kipindi hicho" Alisema Mhe.Mwanzinga -Diwani Kata ya Matola.


Akitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali Mjumbe  wa kamati ya Fedha na Utawala Michael Uhahula Diwani wa kata ya Yakobi Amesema awamu hii Wamekuwa wakali katika usimamizi wa mapato na ndio maana wamefikia hatua nzuri katika makusanyo.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick

Naye Mjumbe wa kamati ya Fedha Nestory Mahenge Ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amesema mitambo ya ujenzi ya Halmashauri hiyo imekuwa ikizingatia Taratibu katika ukodishaji na wanakwenda vizuri.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI