Na Shomari Binda-Musoma
UJENZI wa " High School's na ujenzi wa maabara ya masomo ya sayansi unaendelea kwa kasi katika jimbo la Musoma Vijijini.
Akizungumza na Matukio Daima leo april 8 mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema mahitaji makubwa ya sasa ya dunia ni kuongeza wataalamu kwenye nyanja za sayansi, teknolojia na ubunifu (science, technology and innovation, STI).
Amesema msingi mkuu wa wataalamu wa aina hiyo ni masomo ya sayansi kuanzia shule za awali hadi kidato cha sita ambapo jimbo la Musoma Vijijini ametaja kutekeleza miradi kadhaa ikiwa ni sehemu ya kupata wana sayansi wengi
Muhongo amesema kila sekondari iliyoko jimboni humo inatakiwa kuwa na maabara tatu za masomo ya fizikia, kemia na baiolojia sekondari zote za Kata na binafsi
Amesema wamekusudia kuongeza idadi ya " High Schools" ambapo kwa sasa ipo Kasoma High School iliyopo Kata ya Nyamrandirira yenye masomo ya HKL, HGL na HGK Suguti High School iliyopo
Kata ya Suguti Itakayo funguliwa julai 2025 yenye masomo ya PCM, PCB na CBG pamoja na Mugango High School iliyopo Kata ya Mugango ambayo pia itafunguliwa julai 2025 yenye masomo ya CBG na EGM na kushauri yaongezwe masomo ya PCM na PCB.
Mbunge huyo amesema matayarisho ya " high school ya Mtiro iliyopo Kata ya Bukumi tayari bweni, umeme na maji ya bomba na maabara 3 za masomo ya sayansi zinakamilishwa. Shule nyingine zinazoendelea na ujenzi ni pamoja na Makojo High School Kata ya Makojo tayari maabara mbili zipo, maji ya bomba na umeme na inakamilishwa maabara moja iliyosalia. "Bugwema High School
Kata ya Bugwema maabara tatu zipo umeme, maji ya bomba yanasubiliwa mradi na bweni linajengwa.
" Kiriba High School
Kata ya Kiriba,Nyakatende High School
Kata ya Nyakatende na Etaro High School
Kata ya Etaro zipo kwenye hatua tofauti za kukamilishwa",amesema
Wachangiaji wa ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari hizo ni pamoja na serikali Kuu,halmashauri,Wanavijiji na vongozi wao,mbunge wa jimbo,mfuko wa jimbo pamoja na wamiliki wa sekondari za binafsi
Aidha mbunge huyo amewaomba wadau mbalimbali wa elimu na kuwakaribisha kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi
0 Comments