Header Ads Widget

KUWA SIMBA HADI RAHA ONA YAIGAGADUA AL MASRY 4-1

 


Na Zuhura Zukhery, Matukio Daima, Iringa

Club ya soka ya Simba imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya kuiondoa Al Masry ya Misri kwa mikwaju ya penati 4-1 kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Simba sports club katika mchezo wa kwanza nchini Misri ilikubali kichapo cha mabao 2-0, ambapo Jijini Dar es Salaam imefanikiwa kurudisha mabao yote yalirudishwa kupitia kwa kiungo mshambuliaji Elie Mpanzu na straika wao Steven Mukwala.

Matokeo hayo yalifanya timu hizo kusomeka magoli sawa ubaoni na ili kupata timu yakufuzu ziliingia katika mikwaju ya penati ambapo Shomari Kapombe alifunga penati ya ushindi 


Umahiri wa mlinda mlango wa club Moussa Camara wa kuokoa kuokoa mikwaju miwili ya penati umepelekea mlinda mlango huyo kuibuka nyota wa mchezo


Utakumbuka kuwa kabla ya Mchezo wa leo, clab ya simba ilipewa jina la utani la mwakarobo na watani wao wa jadi Club ya Yanga kwa kushindwa kuvuka robo fainali mara kwa mara.


Simba imecheza robo fainali mara 7 kabla ya robo fainali hii ya leo, ambapo katika robo fainali zote saba ilifanikiwa kuvuka mara mbili pekee katika hatua hiyo.

 

Utani wa jadi wa timu za soka za Simba na Yanga umekuwa ukinogeshwa na maneno na tambo za mashabiki wa timu hizo,


Maumivu wanayopitia simba sports club katika soka la Tanzania furaha ya mashabiki na matumaini wakayawekeza katika   Kombe la Shirikisho la CAF lakini huko kote wakaishiwa kupewa jina la "Mwakarobo" ambalo liliwaumiza kutokana na historia ya timu hiyo kuishia katika hatua za robo fainali za kombe hilo.

 

Leo  Aprili 9 2025, Simba wamejitoa katika katika jina hilo la maudhi la mwaka robo baada ya kujitupa dimba la Benjamin Mkapa kurudiana na Al Masry, na kuichapa 2-0 na kufanya matokeo kuwa 2-2, kabla ya kwenda katika mikwaju ya penati na kushinda mikwaju 4-1.

Hongera simba kila la kheri kwa hatua zinazofuata.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI