Header Ads Widget

JIMBO LA NZEGA MJINI SEHEMU YA TATU


Makala iliyopita nimegusia sekta ya elimu na nikaeleza umuhimu wake katika kuiendeleza jamii katika nyanja zote ikiwemo kujitambua kwa jamii, leo nihitimishe  hoja hii ya elimu katika mambo mawili tu kati ya mengi, moja alilokuwa ameliahidi bwana Hussein Bashe mwaka 2015, kuwa yale majengo ya kambi la wachina waliyojenga wakati wanatengeneza barabara ya kutoka Nzega kwenda Tabora, aliahidi atafanya kuwa veta ili vijana wasio na ujunzi waende kujifunza fani mbalimbali.

Lakini matokeo yake mpaka sasa hakuna cha veta toka 2015, badala yake majengo yale yamegeuzwa kuhifadhi na kuuzia maji.

Hivyo ahadi ile ilikuwa ni uongo na ulaghai kwa wananchi wa Nzega.n

Uongo mwingine ni ile shule inayoitwa "Bashe sekondari" iliyopo kata ya Mwanzoli, amepiga propaganda na uongo kwamba shule ile ameijenga yeye, huo ni uongo, shule ile imejengwa na Halmashauri ya Mji, lakini akajimilikisha kuwa yeye ndiye kaijenga na kusema atawasomesha wasichana kwa gharama zake.

Lakini pamoja na kujinasibu vile imefika mahali uendeshaji wa shule ikawa changamoto kubwa, wazazi wakatakiwa wachagie gharama na bado ikabidi waiombe serikali kuu kuchagia gharama za uendeshaji.


Kilichotokea ni kwamba serikali kuu ilitoa sharti la kuirejesha shule hiyo mikononi mwa serikali kuu, iondoke kuwa chini ya Halmashauri.

Masharti hayo maana yake ni kwamba, shule hiyo ikishakuwa mikononi mwa serikali kuu sio tena itaendelea kuwa chini ya Halmashauri kama kitegauchumi, kwamba mwanafunzi ye yote nchini ataruhusiwa kuja kusoma pale, tofauti na sasa wanaotakiwa kwenda kusoma pale ni wale wanaotokana na Halmashauri husika tu.

Imekuwa ngumu kuirejesha mikononi mwa serikali kuu kwa kuwa jamaa amewafinyanga Halmashauri wamekubali shule iwe chini ya "Bashe sekondari" kwa manufaa yake binafsi ya kisiasa.

Watoto wa masikini wamezubaishwa pale na changamoto kibao wanazopitia wao na wazazi wao.

Tunasema elimu bora ni jawabu la ajira kwa vijana, kinyume chake huyu bwana anatumia elimu kama kete ya kisiasa kwa kuwadanganya wananchi.

Basi angeishia kudanganya wananchi kwa kuwaahidi uongo, lakini cha kushangaza ni kwamba kila wanapopatikana wadau wa elimu kuchangia mahitaji ya wanafunzi na waalimu shuleni, Mbunge anamzuia mkurugenzi asiruhusu.

Nimetolea mfano huu katika makala ya pili ambao ni wa kweli, kwamba Hussein Bashe alimzuia mkurigenzi  naye akawapiga marufuku waalimu wakuu kupokea misaada ya wadau wa elimu kuchangia mahitaji ya wanafunzi na waalimu shuleni kama ule wa compyuter, photo copy mashine na hata ujenzi wa majengo shuleni.

Yaani Mbunge anaahidi uongo, wanapatikana wadau wa kufanya kweli kutatua changamotk za wanafunzi na walimu, lakini mbunge anawazuia na wala hafanyi alichowazuia wadau wasifanye.

Hivi huyu Mbunge utasema ana nia njema na maendeleo ya wananchi?

Tukutene ya nne, sekta ya ujenzi - miundombinu, biashara na uchumi wa Nzega.

Kwiyeya Singu. 0784977072

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI