Header Ads Widget

DC MBEYA AWATAKA VIJANA KUWA WAAMINIFU KUJIJENGA KIUCHUMI

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka vijana kuwa waaminifu na kujiamini ili kuendesha maisha yao kupitia fursa mbalimbali kutoka Serikalini ili kujiimarisha kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya, amesema hayo wakati akifungua kongamano la vijana kutoka kata mbili za Nsalala na Utengule Usongwe mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya waliokutana katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa mwito wa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Erica Yegella.

Malisa amesema vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo hivyo wanaweza kutumia elimu walizozipata kubuni miradi mbalimbali na kuifanya bila kuwa na ulazima wa uwepo wa fedha ilimradi kama watakuwa waaminifu.


"Na hapa kuna tatizo kubwa kwenye eneo hili (la vijana) kwa sasa suala la uaminifu kwa vijana wengi ni tatizo kubwa yaani ukifika getini kwa mtu ukiingia tu unaanza kuangalia hivi hii nondo haiwezi kutoka hapa! Ndio maana mtu akija hapa kutoka Kenya anafungua Hotel yake anaona bora achukue wa-Kenya au achukue watu wa nchi anayotoka kwasababu vijana wengi wamekosa uaminifu", amesema Malisa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Erica Yegella, amesema aneamua kuwaita vijana hao wasomi wa ngazi na tasnia mbalimbali ili kuwaonyesha namna ambavyo Halmashauri yake ya Mbeya ina fursa mbalimbali kwao (vijana) ikiwemo mikopo ya asilimia nne kwa kundi hilo ili kujiimarisha kiuchumi kupitia miradi wanayoifanya kwa mtu mmoja mmoja au kwa kundi la vijana.


Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Agness Elkunda, amesisitiza suala la uaminifu kwa vijana kwa kurudisha mikopo yao kwa wakati na kwa uaminifu ili kunufaisha wakopaji wengine.



Baadhi ya vijana wamesema wamenufaika na kongamano hilo na kuushukuru uongozi wa Halmashauri ya Mbeya kwa kuwaonyesha fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI