Header Ads Widget

CCM MUSOMA VIJIJINI YAKUBALI UTELEZAJI WA ILANI YA MBUNGE MUHONGO NA DIWANI MAGOMA

 



Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Mapinduzi ( CCM) wilaya ya Musoma Vijijini imekubali kazi inayofanywa na mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo  na diwani wa Kata ya Mugango Charles Magoma.

Mwenyekiti wa chama hiyo Denis Ekwambi maarufu kwa jina la ( Ruto) amesema kazi za viongozi hao źinaonekana kwenye utekelezaji wa ilani na kutimiza majukumu yao.

Kauli hiyo ameitoa leo aprili 25,2025 kijijini Kurwaki Kata ya Mugango wakati wa sherehe za ufunguzi wa shule mpya ya sekondari ÿa Kumbukumbu ya Profesa David Masamba.

Amesema mbunge Profesa Sospeter Muhongo amekuwa mfano wa kuigwa katika kuwaletea maendeleo wananchi yakiwemo ya kielimu.


Ekwabi amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan analeta fedha za utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa shule lakini mbunge amekuwa mfatiliaji wa karibu.


Amesema kwenye uchaguzi wanakwenda na Samia kwenye nafasi ya Rais na ubunge na udiwani Muhongo na Magoma wamefanya vizuri.


" Naomba mje niwashike mkono maana mmefanya vizuri na Chama cha Mapinduzi kinataka viongozi wa namna hii ambao haitakuwa TABU kuwanadi kwenye uchaguzi.


" Tumshukuru pia mkurugenzi wa halmashauri na mhandisi wake kwa usimamizi mzuri wa miradi na leo tunaona matunda yake ikiwemo shule hii"amesema.


Akikabidhi shule hiyo kwa wananchi baada ya kuitembelea na kukagua,mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewataka wananchi kuitunza na kuwa marafiki wa walimu ili wawafundishe wanafunzi kwa ari.


Amesema asante na shukrani zimfikie Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kitoa kiasi cha milioni 584 kuijenga shule hiyo na kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kutembea umbali mrefu kwenda masomoni.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema kiongozi bora anapimwa kwa kushiriki shughuli za maendeleo na kusema watakaokuja kwaajili ya kuomba uongozi wapimwe kŵ namna walivyoshiriki shughuli za maendeleo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI