Na Shomari Binda-Musoma
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Commonity Church Tanzania ( NLGCCT ) Dr.Daniel Ouma amemuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kusamehe wale wenye makosa kupitia Pasaka hii.
Ombi hilo amelitoa leo aprili 20,2025 kwenye mahubiri ya ibada ya Pasaka kwenye Kanisa Kuu lililopo Kigera Bonde la Baraka Manispaa ya Musoma.
Amesema sikukuu ya zpasaka inaendana na msamaha na kumuomba Rais Samia kusamehee wale wate waliokosea na hata walioko magerezani wenye kustahili kusamehewa.
Askofu Dr.Dao amesema anaamini moyo wa huruma na upendo aliokuwa nao hivyo anaeeza kusamehe kama ambavyo amekuwa akisamehe kwenye sherehe mbalimbali.
Amesema kwenye sherehe za uhuru disemba 9 2024 kupitia sherehe za uhuru alisamehe zaidi ya wafungwa 1500 hivyo hata kwenye Pasaka hii anaweza kusamehe wale waliokosea na wakaendelea kujenga taifa pamoja.
Kiongozi huyo wa imani amesema anajua wapo waliokosea na kuhitaji kusamehewa hivyo anawaombea msamaha ili waweze kusamehewa.
" Tupo kwenye ibada ya pasaka baada ya kumalizika funga ya kutubia ya Kwaresma tunawaombea wakosaji wote waweze kusamehewa.
" Pasaka ni sikukuu ya kusamehe na tunajua wapo waliokosea serikali tunamuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na moyo wake wa huruma na upendo aweze kusamehe kupitia Pasaka hii",amesema.
Aidha Askofu huyo amewaomba wananchi kuendelea kuheshimu mamlaka za serikali kwani hata maandiko yanasema hivyo.
Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anapaswa kuheshimiwa kwa kuwa ni kiongozi wa nchi pamoja na mamlaka nyingine wakiwemo wakuu wa mikoa,wilaya na viongozi wengine.
Ibada na sherehe za Pasaka zimeadhimishwa duniani kote na waumini wa dini ya kikristo baada ya kumalizika funga ya tobacco ya Kwaresma.
0 Comments