Header Ads Widget

ALLY HAPI APOKEA WANACHAMA WAPYA TOKA VYAMA VYA UPINZANI MUSOMA

 

Na Shomari Binda-Musoma 


KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ally Hapi amepokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani mjini Musoma wakidai kulidhishwa na kazi iliyofanywa na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan.


Wanachama hao wamepokelewa leo aprili 5,2025 kwa niaba yake na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Ally Kassim Mandai kwenye maadhimisho ya wiki ya wazazi kwa wilaya ya Musoma mjini.


Akizungumza mara baada ya kuwapokea wanachama hao kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo amewapongeza wanachama hao kwa uamuzi walioufanya wa kujiunga na chama hicho.


Amesema kuona na kuridhishwa na kazi zilizofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuamua kujiunga na chama hicho ni jambo jema na kuwakaribisha.


Mjumbe huyo amesema kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ameahidi kuwapa ushirikiano wote kama wanachama wengine wa chama hicho.


" Nichukue nafasi hii kuwakaribisha sana ndani ya Chama cha Mapinduzi na niwapongeze kwa kuziona kazi zilizofanywa na mheshimiwa Rais na kujiunga nasi.


" Mjisikie mpo nyumbani na mtapata ushirikiano kama wanachama wengine mliowakuta ndani ya chama na twende tukashirikiane kwa pamoja",amesema.

Awali akitoa salamu za Katibu Mkuu Ally Hapi Mjumbe huyo amesema amemuagiza kuja kusisitiza ushirikiano na kupendana kwa wanachama wote wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao.



Mmoja wa wanachama hao waliohamia chama hicho Desemund Methusela aliyekuwa mgombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA)kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 Kata ya Kigera amesema kazi zilizofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zimewavuta kujiunga na chama hicho.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mgore Miraji amesema wataendelea kusimamia maadili mazuri ya watoto ili kujenga jamii bora.

Licha kuzungumzia maadili ya watu amesisitiza suala la ushirikiano na kupendana na kumsemea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kazi nzuri alizozifanya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI