Na Gabriel Kilamlya Habari na Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa Amemuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe kuhakikisha anapeleka Fedha za kukamilisha miundombinu ya elimu katika shule ya Sekondari ya Wasichana Njombe iliyopo Usalule kutokana na baadhi ya majengo Likiwemo Bwalo la Chakula kutokamilika.
Majaliwa ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua shule hiyo ambayo ina kidato Cha kwanza hadi cha tano kwa watoto wa kike huku baadhi ya miundombinu ikiwa haijakamilika.
Wakati Waziri mkuu akieleza juu ya maboresho ya Sera mpya ya elimu huku akisisitiza kuwa Elimu ya Msingi kuwa ni ya lazima kwa kila Mtoto kwa shule za Msingi hadi Sekondari, Wathibiti ubora wakuu wa Shule kutoka Wilaya ya Wanging'ombe,Makambako,Halmashauri ya wilaya ya Njombe na Njombe mji wameitaka Jamii kutambua uwepo wa Elimu ya awali inayofundisha ujuzi mbalimbali ikiwemo Kilimo,Michezo,Ushonaji,Useremala na hata umeme .
Kwani hii itasaidia wanafunzi kuhitimu Elimu ya Sekondari wakiwa na ujuzi na Maarifa yatakayowawezesha kujimudu katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kutumia ujuzi huo kujiingizia kipato kupitia utaalamu walioupata shuleni.
Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Dokta Festo Dugange Naibu Waziri Tamisemi anatumia fursa hiyo Kuishukuru serikali kwa kupeleka Zaidi ya shilingi bilioni 15 kwenye sekta ya elimu wilayani humo.
Mary Ndimbo na Neema Kambarage ni wanafunzi wa kidato Cha Tano mchepuo wa Sayansi ambao wanashukuru kwa kuboresha mazingira ya shule hiyo huku wakiomba Kukamilishwa kwa miundombinu yote hususani Bwalo la Chakula.
Kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Dokta Peter Nyanja Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Zacharia Mwansasu amesema Zaidi ya shilingi bilioni nne zilijenga shule hiyo Ambayo hadi sasa Ina Zaidi ya wanafunzi wa kike 400 na wanaendelea vyema huku Akisema mapato ya ndani yatatumika kujenga baadhi ya miundombinu Ambayo haijakamilika.
Mhe.Mwansasu Amesema Zaidi ya shilingi Milioni 700 zinahitajika kukamilisha ujenzi wa Miundombinu mbalimbali katika shule hiyo na kwamba katika kipindi Cha miezi miwili ijayo ujenzi huo utafikia hatua nzuri.
0 Comments