Header Ads Widget

WASIRA: CCM, CHAMA KINACHOSHUGULIKIA KERO ZA WANANCHI.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira, akiongea na Wana CCM Maswa (hawapo pichani).


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira amesema kuwa CCM ni Chama kinachoshughulikia kero za Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, ameeleza kuwa CCM siyo chama Cha kulinganisha na vyama vingine nchini ikiwemo vya ACT Wazalendo, CHADEMA, UDP, NCRRM Mageuzi na vinginevyo kutokana na ukongwe wake.


Ameyasema hayo leo mara baada ya kuwasilisha kwenye ziara ya kikazi Mkoani Simiyu, wakati akiongea na wakazi wa Maswa kwenye Mkutano uliofanyika ukumbi wa Halmashauri wilayani Maswa.


Wasira amesema serikali ya Dk. Samia kupitia Chama Cha Mapinduzi, imefanya kazi kubwa sana ya kutatua kero za Wananchi.


"Ndani ya miaka minne ya Rais Dk. Samia, katika sekta ya Elimu ya msingi na sekondari,  yamejengwa madarasa 381 kwa miaka minne ambapo katika shule za msingi kuna madarasa 49 na sekondari yako 332" amesema na kuongeza.


"Kabla ya Samia kulikuwa na Zahanati 43 wilayani Maswa na leo zimefika 53 kwani zimeongezeka zahanati 10 na vituo vya Afya vinne vimejengwa...Maji, yameongezeka, adha ya kuwatua ndoo kichwani imetekelezwa sasa inahamia kwenye kazi na Utu".


Wasira amewataka viongozi wa CCM ngazi ya matawai na kata kuhakikisha wanaweka maslahi ya Chama mbele, huku akiwaonya baadhi ya watu walioanza kusambaza hela (kugawagawa hela), kwa ajili ya kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.

"Tunataka kuwa na Chama kinachoheshimika, siyo kuwa na genge la Chama kinachogawana hela, tunatakiwa tujenge Chama Cha watu wanaoheshimika...CCM nguvu yake ni Umoja, tunapogombana wapinzani wanapita katikati yetu" ameonya Wasira.


Katika hatua nyingine, Wasira amefafanua kuwa kazi ya Kujenga nchi ni kazi ngumu hivyo kuna hatua kadhaa zimefanyika ikiwemo ujenzi wa Barabara za lami nchi nzima.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amesema Chama na serikali Mkoani humo wanafanya kazi vizuri sana na wanashirikia na kufanya miradi mingi ya Maendeleo kutekelezwa kwa kiwango kizuri.


Awali, Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki ameipongeza serikali ya Dk. Samia kwa kutekeleza miradi ya Maji katika Jimbo lake na kuwatua akina mama ndoo kichwani.


Elimu, kata zote 17, Zina Shule za Sekondari Bora na nzuri, zingine Shule mbili, mwambie tunamshuku Kwa shule mpya alizotujengea, Samia ni mama wa nguvu.


Naye Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Stanislaus Nyongo ameeleza kuwa miradi mingi ya Maji imetekelezwa na zana ya kumshusha mama ndoo kichwani inaenda kutimilika kwenye kata zote 19 Jimboni humo.


Mwisho.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI