Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali ya Mkoa wa Njombe imeahidi kutoa fedha za mahitaji yote muhimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Viziwi Zilizopo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe kwa ubia na Serikali.
Ahadi hiyo inatolewa na Katibu tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary wakati akikabidhi misaada mbalimbali na fedha zaidi ya shilingi milioni moja kupitia Jukwaa la Wanawake waliokwenda kuwaona watoto hao ikiwa ni wiki ya kuelekea Kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani.
Awali Mkurugenzi wa kituo Cha Elimu Cha Viziwi mkoani Njombe Mchungaji Alphonce Ngavatula Amesema miongoni mwa changamoto za kituo hicho ni pamoja na Kushindwa kumudu gharama za uendeshaji kutokana na myumbo wa Uchumi duniani uliosababisha wafadhili kujitoa na kuwalazimu kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoa wa Njombe Anna Mwalongo anasema siku ya wanawake Ilianzishwa baada ya kubaini uwepo wa Mfumo dume katika jamii na hivyo wameamua kutumia wiki hii kutembelea makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa Kituo Cha Viziwi na kuwapa misaada.
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa Kila Machi 8 ya Mwaka na kwa mkoa wa Njombe maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika huko Wilayani Makete.










0 Comments