Header Ads Widget

WANAWAKE NJOMBE DC WASEMA UKATILI BADO UPO


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati siku ya mwanamke ikitumika kutathmini Maendeleo na Uchumi wa Mwanamke Duru zinaripoti kuendelea kuwapo kwa mkwamo wa baadhi ya mambo ikiwemo Haki za kumiliki mali pamoja na Migogoro katika familia mkoani Njombe.

Taarifa ya Maendeleo ya Wanawake na watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe iliyosomwa na Ledempta Kagaruki, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Katika Maadhimisho ya siku ya mwanamke Halmashauri hiyo yaliyofanyika katika Kijiji Cha Matiganjola imeeleza kuendelea kupunguzwa kwa migogoro mbalimbali inayowakumba pamoja na kuaminiwa katika uongozi na hii imechagizwa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuendelea kupigania Haki sawa.

Kagaruki amesema bado kuna Ukatili wa kukosa haki ya Kumiliki ardhi,Kurithi wajane,Ndoa za Utoto zinazowakosesha watoto haki ya kupata elimu pamoja na watoto kuendelea kutumikishwa kwa kazi za ndani na mashambani.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa CCM UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema huu sio wakati wa kumtenga mwanamke wala Mtoto wa kike katika nyanja mbalimbali na hii ndio sababu ya kuanzishwa kwa siku hiyo ili kupigania maslahi yao.

Madiwani wa viti Maalumu Tarafa ya Lupembe Getrude Chungwa na Neema Mbanga wamesema Wanawake mkoani Njombe wanapaswa  kutambua kuwa suala la haki sawa ni katika masuala ya Utawala na uongozi na sio katika familia kwani hii itasaidia kudumisha amani na Upendo katika ndoa na Taifa kwa Ujumla.

Kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Tecla Sadala  Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu Amesema wazazi wanapaswa kuwapeleka watoto shule ili kuepukana na changamoto za ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Mgeni wa Heshima katika Maadhimisho hayo Valentino Hongoli Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe anasema serikali Imeendelea kuweka usawa katika masuala mbalimbali na hivyo maeneo Ambayo bado yataendelea kushughulikiwa.

Kauli mbiu ya siku ya wanawake Duniani kwa Mwaka huu ni "Wanawake na Wasichana 2025 tuimarishe Haki usawa na uwezeshaji".









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI