Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.
WANANCHI wa Mtaa wa Mbwamaji Geza ulole uliopo Kata ya Somangila Wilaya ya Kigamboni wamemuomba Mwenyekiti wa Mtaa huo Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' kuwapazia sauti kufikisha maombi ya changamoto za Mtaa huo kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ya upatikanaji wa Shule, na ujenzi wa Miundombinu ikiwemo barabara na mitaro.
Wananchi hao wametoa rai hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki ulioitishwa na Mwenyekiti Mhe Yohana Luhemeja uliokuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo ajenda kuu ya ukosefu wa Shule ya Msingi Mtaa wa Mbwamaji, Kuboresha Miundombinu ya barabara huku Ajenda zingine zikiwa ni usafi wa mazingira, Ulinzi na Usalama, Umaliziaji wa upimaji shirikishi (Ardhi) na Ukarabati wa jengo la Serikali ya Mtaa.
Wananchi hao walipaza sauti juu ya kuboreshwa miundombinu ya barabara kwa kuwa barabara zote za mtaa ni mbovu toka 2014 hadi sasa hakuna barabara iliyo tengenezwa kwa kiwango cha changarawe kila mwaka Wananchi wanaomba kwa Mkurugenzi ila hakuna mafanikio.
Hata hivyo wamesema Serikali imewasahau wananchi wa mtaa wa Mbwamaji Geza ulole hata ilani ya CCM hakuna mradi hata mmoja kwa mwaka 2025 na kuomba majibu kwa mkurugenzi kuhusu kutengenezewa mtaro mmoja na barabara Nne ama mbili kiwango cha rami.
Wananchi hao, wamebainisha kero hizo zimekuwapo muda mrefu hivyo wameomba Mwenyekiti huyo mpya aweze kuzitatua huku zile kubwa aziwasilishe kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.
...Wananchi Wamekuwa watu wa kuomba miaka yote bila kupata utatuzi wa changamoto zao,
Hivyo wameonelea kupaza sauti kwa Mhe. Rais Samia kupitia kwa Mwenyekiti ili wapate kusaidiwa.
Awali, Wananchi hao wamempongeza Mwenyekiti Mhe Yohana Luhemeja kwa kuitisha mkutano huo kwani imekuwa tofauti na Uongozi uliopita 2019 hadi 2024 ambao hawakuitisha mkutano wa wananchi.
Nae Mwenyekiti Mhe Yohana Luhemeja akijibu kero hizo za Wananchi, amesema:
"Masuala kama Shule, Mtaro, Barabara tayari nilisha wasilisha kwenye kamati ya Maendeleo ya Kata pia Ofisi ya Mtaa tulishaandika barua kwa Mkurugenzi tunasubiri majibu, Ninahakika Rais wetu ni msikivu watayafanyia kazi kupitia watendaji wake wanaomsaidia katika ngazi zote.
Aidha, Mhe.Yohana Luhemeja amebainisha kuwa, awali shule ya Msingi mtaa wa Mbwamaji hapo awali ulikuwa na shule ya Msingi Geza Ulole iliyo hamishiwa Mtaa wa Kizani kwa kupisha eneo hilo ambalo linatarajiwa kujengwa soko /kiwanda cha samaki ambapo hata hivyo Wananchi wamesema mabadiliko hayo hawakushirikishwa pamoja na hayo wananchi wamerudia tena ombi la kujengwa shule mpya kwenye eneo walilo lipitisha ndani ya Mtaa huo wa Mbwamaji.
Wananchi mtaa wa Mbwamaji una wanafunzi zaidi ya 750 ambao wanasoma nje ya mtaa huo hali inayopelekea watoto kupata shida hasa wakati wa masika.
Mbwamaji Geza ulole ni miongoni mwa mitaa kongowe nchini yenye kubeba historia Dar es Salaam.
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Mbwamaji Geza ulole wakifuatilia Mkutano huo
0 Comments