Header Ads Widget

WANANCHI MANISPAA MOROGORO WAOMBA HUDUMA ZA AFYA BURE KUTOLEWA KILA WAKATI

 

📌 Ni baada ya wanawake wa Hospitali ya Mzinga pamoja na Wanawake kada ya afya Manispaa Morogoro kutoa huduma hiyo bure

Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio DaimaApp 


WANANCHI wa Manispaa ya Morogoro wameomba kuwepo kwa Kambi za tiba kila wakati Ili kuwasaidia kupata huduma za afya kwa haraka na bila usumbufu.

Walitoa Rai hiyo walipohudhuria Kambi ya huduma za kitabibu zinazotolewa bure na Wanawake  wa Hospitali ya Shirika la Mzinga na Kikosi cha Jeshi Mazao kwa pamoja na Wanawake kada ya afya wa Manispaa ya Morogoro,huduma inayoendelea kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Sabasaba mkoani Morogoro.



Farida Maulidi mkazi wa Konga alisema" Nimepata vipimo  vyote nilivyohitaji bila usumbufu the tena bure,wananchi tunahitaji huduma hizi kila wakati Ili kujua afya zetu,"


Naye Jostina Senyagwa alisema kuwepo kwa Kambi za matibabu kuwasaidia wananchi kujua hali zao za afya kwani ni rahisi kufika kwenye Kambi hizo ukilingsnisha na hospitalini ambapo wamekuwa wakichukua muda mrefu kupata huduma.


"Huduma hapa ni mzuri na za haraka, tunafanya vipimo na majibu yako hapo hapo tofauti na hospitali unakata muda marefu kwenye foleni ukitoka hapo umechoka zaidi,"alisema Senyagwa.


Wananchi hao walisema idadi kubwa ya wagonjwa wanakwenda hospital wakiwa wakiwa wamechelewa kutokana na kutofanya vipimo.


Walisema ikiwa kutakuwa na Kambi za vipimo kwenye maeneo yao wengi watajitokeza ili wanaogundilika wanaanza tiba mapema.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kambi hiyo, Kaimu mganga mkuu wa Wilaya Dk Ester Masaule alisema nia ya serikali ni kuwarahisishia wananchi  upatikanaji wa huduma Kinga na vipimo ili waweze kujua Hali ya afya zao mapema.

"Zoezi hili linawasaidia wananchi kupata vipimo bure na wanaogunduli na matatizo wanaanzishiwa huduma za awali za matibabu,"alisema Dk Masaule.

Mratibu wa Kambi hiyo ya siku tano,Demantiria Mushi alisema zoezi hilo la kutoa huduma bure za matinabu ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo kitaifa yatafanyika Jiji Arusha ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Katika Kambi hiyo inatoa huduma zaidi kwenye vipimo Bure ni za upimaji wa macho, sukari, shinikizo la damu, ukimwi, saratani ya shingo ya kizazi maralia, homa ya ini.mkoani

Alisema wanaogundilika kuwa na tatizo wanapata ushauri na wanaanzishiwa huduma ya awali ya matibabu ili waendelee na kliniki.

Kambi hiyo imeandaliwa na wanawake wa hospitali ya shirika la Mzinga na wanawake wa kada ya afya wa manispaa ya Morogoro inajumuisha utoaji wa vipimo mbalimbali na tiba ya awali kwa wanaogundilika na changamoto za afya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI