Na Habari na Matukio App
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam wameonyesha umahiri wa hali ya juu kiasi cha kuwashangaza maofisa wa Umoja wa Mataifa (UN) na wa Ubalozi wa Rwanda walipokuwa wakijibu maswali na kuhusu mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
Maofisa hao walitembelea shule hiyo hivi karibuni kwa lengo la kuzungumza nao na kuwaeleza kuhusu yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 ambapo wanafunzi hao walipata muda wakuuliza maswali na kupatiwa majibu.
Pia maofisa hao waliwauliza maswali wanafunzi hao ambao walionyesha umahiri mkubwa katika kuyajibu hali ambayo iliwashangaza maofisa hao kutokana na udogo wa wanafunzi hao wa shule ya msingi na awali.
Kila tarehe 7 Aprili Rwanda imekuwa ikiadhimisha mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo idadi kubwa ya watu wa kabila la watusi waliuwawa na wa kabila la wahutu wenye msimamo wa wastani.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Habari wa Umoja wa Mataiafa (UN),Nafisa Didi alisema wameshangazwa na umahiri wa wanafunzi hao kujibu maswali kuhusu mauaji ya kimnbari ya Rwanda.
“Kwa kweli tumeshangazwa sana na hatukuamini kwamba wanafunzi wangeweza kujibu kwa umajiri wa kiwango hiki yaani huwezi kuamini kwamba hawa ni wanafunzi wa shule ya msingi kwa uwezo walioonyesha leo,” alisema
Alisema tarehe 7 mwezi ujao ni kumbukizi ya mauji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 ambapo shughuli mbalimbali hufanyika ikiwemo kutoa elimu kwa umma kuhusu kilichotokea.
“Tumeona tuwaelimishe wanafunzi wajue nini kilichotokea na kwanini kilitokea ili wakue wakijua kilichotokea ili mambo kama yaale yasije kutokea tena kwenye jamii,” alisema Didi
“Watoto ni wadogo lakini wameuliza maswali mazuri ambayo yametushangaza kwa umri wao ni wadogo lakini wameonyesha umahiri mkubwa sana kwenye kuuliza na kujibu maswali,’ alisema
Mkuu wa shule ya Hazina, Omari Juma alisema imekuwa kawaida kila mwaka wakati wa kumbukizi ya mauaji ya kimbari maofisa wa UN kuja kuelimisha wanafunzi masuala yaliyotokea wakati wa mauaji hayo.
Alisema ushiriki wa wanafunzi umekuwa mzuri na washiriki wa mjadala huo wameelezea kushangazwa na uwezo ulioonyeshwa na wanafunzi hao.
“Siku imekuwa nzuri sana wanafunzi wetu wameonyesha vipaji vya hali ya juu kiasi cha kuwashangaza maofisa wa UN na Ubalozi wa Rwanda kwa namna walivyomudu kujibu na kuuliza maswali kuhusu mauaji ya kimbari,” alisema Juma.
Mwisho
0 Comments