Header Ads Widget

UWT SAME WAMPONGEZA MBUNGE ZUENA BUSHIRI KWA KUKABIDHI MABATI 50..



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilayani Same mkoani Kilimanjaro umemshukuru Mbunge wa Viti maalum kupitia mkoa huo, Zuena Bushiri kwa kukabidhi mabati 50 kwa ajili ya kupaulia nyumba ya mtendaji wa Jumuiya hiyo ambaye ni Katibu wa UWT wilaya. 


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mabati hayo na Mbunge huyo, Katibu wa UWT wilaya ya Same, Upendo Sankey alisema msaada huo utasaidia kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika mapema na kuhamiwa. 



"Sisi UWT wilaya ya same tunamshukuru na kumpongeza Mbunge Zuena kwa mchango wake huu mkubwa wa mabati kwani ameyaleta katika wakati muafaka ambao tunapambana kuhakikisha nyumba hii inakamilika" Alisema Upendo. 


Awali akikabidhi mabati hayo, Mbunge Zuena Bushiri alisema kuwa, lengo lake ni kuhakikisha anashirikiana na wanachama wa umoja huo na wasio wanachama  kuhakikisha nyumba za makatibu wa uwt wilaya na mkoa wa Kilimanjaro zinakamilika. 



Zuena alisema kuwa, ataendelea kushirikiana na wana ccm na wasio wana ccm kuhakikisha nyumba zinakamilika kwa wakati. 



Aidha alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kutoa fedha nyingi za maendeleo katika wilaya ya Same kwa kipindi chake cha miaka minne. 


"Rais Dkt. Samia ni mtu wa kuigwa katika Taifa hili kwani ameonyesha dhamira yake ya dhati kwa vitendo kila wilaya ametoa fedha nyingi za maendele katika mkoa wetu pekee kwa kipindi chake cha miaka minne ametoa zaidi ya Trilioni moja katika sekta mbalimbali" Alisema Mbunge Zuena.

Mbunge huyo alisema kuwa, kwa sasa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro hakuna wanachomdai Rais Dkt. Samia. 


Aliwataka wananchi kumlipa kwa kumpa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu mwaka huu pamoja na Wabunge na Madiwani wanaotokana na ccm. 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI