TAZAMA TAARIFA YA HABARI LEO MACHI 20/2025 BOFYA LINK HII
Na Matukio Daima Media
Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Iringa Leonard Manoko kurwijilla amesema kuwa katika hali ya utawala ni sahihi Kwa Jimbo la Kilolo kuweza kugawanywa kwaajili ya kuwahudumia watu.
Kurwijila ameyasema hayo hii Leo mara baada ya kutoka katika Kikoa Cha mchakato wa kuligawa Jimbo la Kilolo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kilichohusisha viongozi mbalimbali huku kikiwa kimebeba ajenda Kuu mbili ikiwemo kupitia mapendekezo ya kuligawa jimbo la uchaguzi la Kilolo na kupendekeza kuundwa Kwa halmashauri mpya.
"Sisi kama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tunasema kiutawala ni sahihi kuligawa Jimbo la Kilolo kwasababu ni kubwa japokuwa linakosa vigezo vya kuwa na idadi kubwa ya watu na Kwa ukubwa wa Jimbo la Kilolo kama kweli tunahitaji kuwahudumia watu na kuwafikia watu na Ili watu wapate huduma nzuri bila changamoto ni vizuri kuharakisha maendeleo ya Jimbo la Kilolo na kuligawasha Jimbo hilo"
Pia ameelezea umuhimu wa kugawashwa Kwa majimbo na kuwa jambo hili halipingani kabisa na kauli zao za kusema kwamba kuongeza majimbo kunaongeza nafasi za uongozi ambazo zinaleta matumizi makubwa hivyo kuna umuhimu wa kuwa na majimbo machache Ili kubana matumizi.
"Unapoongeza idadi ya majimbo unapanua uwezekano wa watu kuweza kusaidiwa mapema katika huduma mbalimbali za kijamii kama huduma za hospitalini na hii itasaidia kuondokana na changamoto mbalimbali japokuwa katika hili ni vizuri kuwa na wabunge wengi ambao ni wawakilishi katika Mkoa na hii inatokana ugawaji wa majimbo.
Aidha Kurwijila amependekeza uwepo wa Bunge la Mkoa ambalo litahusika zaidi katika kuwafikia wananchi na kuwahudumia Kwa ukaribu pia Bunge hilo litahusika na kuchakata mambo mbalimbali ambayo atapewa mwakilishi moja kwaajili ya kwenda Dodoma kutuwakilisha kwenye kamati Kuu.
"Mtazamo wetu sisi kama Chama mfano tungekuwa tumeshika Dola hakukuwa na haja ya kuwa na wabunge wengi ambao wanakwenda kujaa Dodoma mpaka nafasi zinataka kukosekana za kukaa wabunge ila wabunge wangeongezeka Ili wawahudumie wananchi lakini wabunge hao sio wale wa kwenda Dodoma bali ni wale wa Mkoa ambao wanachakata mambo mbalimbali ambayo tunakuwa na mwakilishi ambaye atawenda Bungeni kuweza kutuwakilisha".
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ameelezea sababu zilizowafanya kuona kuwa Jimbo hilo la Kilolo linatakiwa kugawashwa
" Yamekuja mapendekezo kutoka Halmashauri na kutoka wilayani sasa ni kazi yetu na sisi kupitia mapendekezo hayo Ili kuona kama tunakubaliana nayo kwasababu Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea muongozo na vigezo vya kugawa majimbo na kata ambacho cha kwanza ni idadi ya watu, ukubwa wa eneo, uchumi wa watu, na hali ya wabunge na jambo kubwa la kuzingatia katika mchakato huu ni hali ya uchumi katika eneo husika na hii kwasasa pengine mnaweza msinielewe lakini Kwa badae ina manufaa makubwa sana"
0 Comments