Header Ads Widget

UCSAF YAFUNGA MTANDAO WA BURE (WIFI) MAENEO SABA NCHINI

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

KATIKA juhudi za kuongeza wigo wa matumizi ya intaneti nchini, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeanzisha huduma ya bure ya WiFi katika maeneo saba ya umma. 

Akizungumza jana jijini hapa, Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda wakati akielezea mafanikio na mwelekeo wa mfuko huo  alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.

Mradi huu unalenga kutoa fursa ya intaneti kwa wananchi, hasa katika maeneo ya huduma na biashara. 

Maeneo yaliyojumuishwa katika mpango huu ni pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Lungemba (Mafinga), Nyerere Square (Dodoma), Ndaki ya Habari na Elimu Angavu (CIVE) katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Soko la Tabora, Kiembe Samaki (Unguja), na Soko la Buhongwa (Mwanza). 




Aidha,Afisa Mtendaji mkuu  wa UCSAF imeongeza  kueleza kuwa huduma hii katika maeneo mengine 17 katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba.

Hata hivyo Amesema Kiwango cha TZS 374 milioni kimewekezwa katika mradi huu, ukilenga kuboresha upatikanaji wa intaneti na kuimarisha huduma za kidijitali nchini.

"Huduma hii inatarajiwa kuboresha mawasiliano, kuongeza ufanisi katika biashara, na kuwezesha wananchi kupata taarifa muhimu mtandaoni, " Amesema 

Sambamba na hilo mtendaji huyo amesema Serikali katika kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano nchi mezi Mei 2023 iliingia mikataba na watoa huduma kwa ajili ya kufikisha mawasiliano maeneo ya vijijini.


"Mradi huu wa ujenzi wa minara 758 ni mradi mkubwa kuwahi kutekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote. Mradi huu ni wa kimkakati ni utafikisha mawasiliano kwenye," Amesema 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI