Header Ads Widget

TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA AFRIKA UZALISHAJI BORA WA KAHAWA AINA YA ROBUSTA.



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


TANZANIA imeibuka kidedea Afrika katika uzalishaji wa kahawa bora aina ya Robusta kupitia kampuni ya Ubumwe Co.Ltd kilichopo wilayani Ngara mkoani Kagera na kuzishinda nchi za Ethiopia, Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, Zambia, Malawi na Ivoricost.

Akizungumzia ushindi huo leo, Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa nchini, Primus Kimario alisema kuwa, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa wazalishaji wa kahawa barani Afrika ambapo katika mkutano huo walishindanisha kahawa mbalimbali.

Amesema kuwa, katika mashindano hayo, Tanzania iliibuka kidedea kwa uzalishaji bora wa kahawa aina ya Robusta Afrika kupitia kampuni ya Ubumwe ambapo ni fursa na wao kama Bodi ya kahawa wanajivunia ubora huo wa kahawa

 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Prof. Aurelia Kamuzora alifurahishwa kuona Tanzania imetoka kidedea kwa uzalishaji wa kahawa bora ya Robusta barani Afrika na kudai kuwa yapo mengi ya kujifunza kutoka katika kampuni ya Ubumwe.

Alisema kuwa, shida kubwa inayotokea katika kahawa hapa nchini ni kuchanganya kahawa kutoka eneo moja na jingine ambapo kitendo hicho huaribu uhalisia na ubora wa kahawa.

Akizungumzia jinsi mashindano hayo yalivofanyika, Afisa Ubora na masoko Bodi ya Kahawa Tanzania, Felix Mlay alisema kuwa, zoezi la mashindano hayo lilianza mwaka jana Disemba ambapo kwa mashindano ya ndani ya nchi na sampuli 73 za kahawa kutoka kwa wazalishaji wadogo na wakubwa.

Alisema kuwa katika shindano hilo washindi walipatikana ambapo kwenda kwenye mashindano ya Afrika zilichukuliwa kahawa tano kwa ajili ya kwenda kushindanisha katika makundi matatu ambayo ni Robusta, Arabika laini na Arabika ngumu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI