Header Ads Widget

UKAME WALETA HOFU YA NJAA WANGING'OMBE NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Ukame mkubwa uliozikumba takribani kata 7 katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe huenda ukasababisha baa la Njaa kutokana na Mazao kukauka kwa kukosa mvua.

Kata hizo ni pamoja na Saja,Wanging'ombe,Kijombe,Uhenga,Ilembula na Luduga ambazo zimekumbwa na Ukame huo licha ya  Mamlaka ya hali ya Hewa Nchini TMA kutahadharisha wananchi kuhusu mvua kubwa zinazoweza kunyesha katika mikoa kadhaa ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Njombe.

Baadhi ya Wakulima Wilayani Wanging'ombe akiwemo Shekh Hamim Mashaka,Neyma Nurdin Editha Magulu na Farida Mwagala  wanasema tangu mvua isimame februari 6 mwaka Huu mazao mengi yakiwemo Mahindi yamekauka hivyo wanaomba serikali kuona namna ya kuwasaidia chakula,mbegu na visima virefu 

Kufuatia ukame kuathiri mazao,wenyekiti wa vijiji akiwemo Gidion Jackson Kutoka Wanging'ombe wanasema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kwasababu ukame unadhohofisha ustawi na usalama wa serikali za vijiji,kwani wafugaji na wakulima wanahama kufuata maeneo rafiki kwa shughuli zao

Kwa upande wake afisa kilimo na ufugaji kata ya Saja Mosi Adam pamoja na mtendaji wa kata ya Wanging'ombe Geofrey Mhufi wanaeleza jitihada wanazochukua ili kusaidia wakulima.

Diwani wa kata ya Saja Andrew Mangula anasema njia pekee ya kuokoa kilimo na mifugo ni kuchimbiwa visima virefu na mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji.

Ukame huo umezikumba kata hizo ambazo zipo ukanda wa Joto wa Wilaya ya Wanging'ombe ambapo serikali imeombwa kuchukua hatua za haraka ili kuwanusuru adha zinazoweza kutokea kwa wakazi wa wilaya hiyo.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI