Header Ads Widget

TAFORI, TAWIRI KUFANYA MASHIRIKIANO YA KITAFITI KUIMARISHA UHIFADHI WA MISITU NA UFUGAJI NYUKI


Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imefanya mazungumzo ya wazi ya ushirikiano wa pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) katika tafiti za maeneo ya uhifadhi ya Misitu ya asili na ufugaji Nyuki.

Mashirikiano haya yatawaleta pamoja watafiti kutoka Taasisi zote mbili kufanya kazi kwa pamoja katika utafiti na kubadilishana uzoefu, kuongeza ujuzi na maarifa ili kubaini maeneo ambayo hayajafanyiwa utafiti katika Sekta ya Ufugaji Nyuki na Hifadhi za Misitu ya Asili ili kuepuka kurudiwa kwa baadhi ya tafiti.

Kikao hiki cha mashirikiano kimefanyika Machi 18, 2025 TAFORI Makao Makuu, Morogoro kikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAFORI, Dkt. Chelestino Balama pamoja na Dkt. Julius Keyyu, Mkurugenzi wa Utafiti TAWIRI.

Ushirikiano huo wa pamoja utafungua mlango kwa watafiti kutoka Taasisi zote mbili kufanya kazi na wawekezaji katika sekta ya utalii ikolojia na uhifadhi Misitu, kujifunza matumizi ya teknolojia, uwekezaji kwenye ufugaji Nyuki, kufanya tafiti katika mazao ya Misitu yasiyotimbao, kuimarisha sera za uhifadhi wa Misitu, na kukabiliana na changamoto ya viumbe vamizi katika Misitu na shughuli za ufugaji Nyuki.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI