Na Habari na Matukio App
UONGOZI wa Shule ya Hazina Magomeni jijini Dar es Salaam umempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa miaka minne ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kuipasha sekta ya elimu.
Kwa mujibu wa Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma Rais Samia amefanya mambo makubwa hususan kwenye elimu ambapo amewezesha wanafunzi wengi kupata elimu ya msingi hadi sekondari.
Shule ya Hazina imekuwa kinara kwa kuwa namba moja kwenye matokeo ya darasa la nne na lasaba kwenye Wilaya ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka mingi.
Alisema Rais Samia amefanikiwa kujenga shule za wasichana za sayansi zinazojulikana kwa jina la Mama Samia kwenye mikoa mbalimbali hivyo kuwapa fursa wasichana wa kitanzania kusomea masomo ya sayansi kwa wingi.
“Hazina mdau mkubwa wa elimu tumekuwa tukiongoza Wilaya ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es Salaam karibu kila mwaka kwa kuwa wakwanza kwenye matokeo ya darasa la saba kwa hiyo tunapoona sekta ya elimu inapewa kipaumbele inatutia moyo sana kamawadau wa elimu,” alisema Juma
“Jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Samia kuinua kiwango cha elimu zinatutia moyo sana sisi wadau wa elimu na tutaendelea kufanya vizuri kwenye matokeo mbalimbali kama mwaka huu kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana wanafunzi wetu wote walipata alama A na kuwa shule bora Wilaya ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema
Alisema Rais Samia amewezesha wanafunzi waliokatisha masomo kwasababu mbalimbali kurejea shuleni hivyo kuwapa fursa ya kupata elimu.
“Sisi kama wadau wa elimu tunafurahi sana kuona shule nyingi za msingi na sekondari zinaendelea kujengwa hapa nchini na amepanua wigo wa wanafunzi wanaopata mikopo ya elimu ya juu hadi ngazi ya stashahada wanapata,” alisema
Alisema hata idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaopata mikopo kutoka bodi ya mikopo imeongezeka mara dufu hali inayowawezesha watoto wa familia maskini kupata elimu.
0 Comments