Header Ads Widget

RC KUNENGE aziagiza TARURA NA TANROADS WAANZE KUSHUGHULIKIA AHADI ZA CCM

 


Mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amezitaka Wakala wa barabara Tanzania  TANROADS na Wakala wa Barabara vijijini na mijini TARURA kushughulikia barabara ambazo tuliwaahidi wananchi katika kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2020 ili zisije kuleta msuko suko mkubwa kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao kwasababu wananchi watapima serikali kwa namna ilivyotekeleza ahadi zake.


Amesema hayo katika mkutano wa bodi ya barabara ya mkoa iliyofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani na kuhusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na wataalamu.



Kunenge alisema ni lazima kuwe na mipango ya utengenezaji wa barabara kwa maendeleo katika mkoa kwa kuanzia kwanza barabara ambazo tuliahidi wananchi kwamba zipi zimekamilika na zipi bado zipo katika utekelezaji na zipo kwenye hatua gani.


"Na tuone na zile barabara ambazo hatujaanza kabisa na tujue kipaumbele ni barabara zipi na zitakamilishwa kutokana na fedha zipi na waheshimiwa Wabunge watueleze ni barabara zipi zipewe kipaumbele hata kama ni tano hata kumi zipi hizo zipewe kipaumbele zitatupa msukosuko mkubwa" alisema RC Kunenge.


"Hata  akija kiongozi mkubwa zitaleta msukosuko mkubwa yaani lazima tuzijue na tuziwekee mkakati kulingana na maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan" alisema Kunenge.


"Angalieni zipi mmezitekeleza na zipi bado hamjazitekeleza na tutoe sababu kwanini hatujazitekeleza na tuone kama tutaenda nazo kwani tunafahamu tuna majukumu mengi lakini hizi barabara tukiziangalia zinaweza kutupa unafuu"


"Lakini tuangalie ni barabara zipi zitatusaidia kukuza uchumi na barabara zipi zitaweza kutupa shida huko mbele kwasababu wananchi wanachangamoto na changamoto zinahitaji fedha lakini ni lazima tuwe na maelezo yanayolenga majibu kwa Wananchi tuwe na maelezo yenye majibu yanayofanana kwa wananchi" alisema Kunenge.

"Tulipofikia hapa tunajipanga kutoa maelezo kwa wananchi ili tumsaidie Mheshimiwa Rais akijakupita huku tuwe na maelezo yanayoeleweka kwa wananchi ikiwezekana tuwe na andiko maalumu tuende nalo hilo" alisema Kunenge .

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amesema wilaya ya kisarawe ina milima mingi sana hivyo hata kiasi cha fedha cha kutengeneza barabara wilayani humo zinakuwa ni ndogo na sasa hivi tunaelekea kipindi cha mvua na kipindi cha kampeni.

Alisema katika kila mikutano anayofanya na wananchi asilimia kubwa ya maswali anayoulizwa ni malalamiko ya madai ya barabara wakilalamikia vumbi kila sehemu hakuna lami.

"Wilaya ile ina miaka ya zaidi ya themanini lakini kuna lami katika kilomita saba tu, hata sasa tunaelekea kipindi cha uchaguzi mkuu kisarawe Mbunge wao na madiwani wao wana wakati mgumu kuliko wakati wowote" alisema Magoti.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI