NA MATUKIO DAIMA MEDIA,IRINGA
Katibu wa Siasa na itikadi ,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Dickson Nathani Lutevele amewakaribisha wafanyabiashara na wajasiriamali wa maeneo ya karibu na wilaya ya mufindi kuweza kuchangamkia fursa kupitia ujio wa katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) cpa amosi makalla ambapo watu takribani 6000 wanatarajiwa kuzulu mkutano huo.
Akizungumza na Matukio daima Tv Lutevele amesema kuwa tangu katibu wa unenezi amosi makala apate nafasi hiyo hii ni mara yake ya kwanza ana kuja mkoani iringa akianzia wilaya ya mufindi na katika hili wamejiandaa vizuri kumpokea hii ikiwa ni pamoja na kuwakaribisha wafanyabiashara kuweza kujitokeza kwa wingi kwaajili ya fursa hii.
”Tunashukuru sana chama chetu kwa hii ratiba kuona kwamba Katibu wetu wa taifa safari hii kwa mara ya kwanza tangu mkutano mkuu ufanyike anapata nafasi ya kuja katika wilaya yetu ya Mufindi na sisi kama chama tumepokea jukumu hili la kumpokea kiongozi wetu na tunatarajia kupokea watu takribani 6000 katika uwanja wa mashujaa uliopo Mafinga na tumeweka uwanja wetu katika mazingira rafiki kwaajili ya watu wote haswa wafanyabiashara na kwa nafasi hii mimi niwakaribishe sana wafanyabiashara na wajasiriamali kuweza kuchangamkia fursa za kibiashara katika uwanja huu”
Lutevele pia ameeleza mambo ambayo wao kama chama wanajivunia katika kipindi hiki ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyofanyika ndani ya miaka minne ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
“katika wilaya ya Mufindi yamefanyika mambo mengi katika kipindi hiki kifupi cha utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwemo mradi wa maji wa Bilioni 40 ambao unaendelea kutekelezwa ambao utachukua eneo kubwa la jimbo la mufindi kaskazini na hili nisema kwa miaka hii minne ya mama yetu katika kila sehemu ambayo wananchi walitamani iguswe basi imegusa hatakama hayajakamilika kwa 100% na kwa upande wa jimbo la mufindi kusini changamoto kubwa zilikuwa ni maji na barabara lakini kwa sasa tunaona miradi hiyo inakwenda kutekelezwa na mingine tayari ishatekelezwa ili kumaliza kero hiyo kwa wananchi”
katika hatua nyingine mwandishi wa habari na mdau wa maendeleo katika mkoa wa Iringa Shalom Robert amesema kuwa ujio wa CPA Amosi Makala katika wilaya ya mufindi unakwenda kufungua wigo mpana kwa vijana kuonesha uwezo wa kisisasa na wa uongozi.
“kwanza ujio wenywewe wa CPA Amosi Makala kwetu sisi kama vijana tayari ni fursa kubwa ukizingatia hata mwenyekiti wetu wa umoja wa jumuiya ya vijana amekuwa akitusisitiza kwamba vijana umefika wakati wa sisi vijana kuweza kwenda kuwatumikia wananchi lakini pia kutumikia chama tukirudi tena katika fursa ujio huu unakwenda kufungua wigo mpana kwa vijana katika kuonesha uwezo wao katika siasa na suala zima la uongozi”
Robert pia amepongeza juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi wa wilaya ya Mufindi chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasssan kwa kuhahakikisha wanakamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara ambayo ilikuwa ni changamoto kubwa sana kwa wananchi wa wilaya hiyo.
0 Comments