Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imefanikiwa kuanzisha huduma mbalimbali za kibingwa na ubingwa bobezi ikiwamo kufanikiwa kuanzisha matibabu ya magonjwa ya ngozi kwa njia ya tiba mwanga na tiba laser ikiwa ni hospitali pekee nchini inayotoa huduma hiyo.u
Huduma hii imekua msada mkubwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya vitiligo na saratani za ngozi ambapo wastani wa wagonjwa 10 hadi 15 wanahudumiwa kwa wiki.u
Aidha, huduma zingine bobezi ni pamoja na za kupunguza uzito, kupandikiza meno bandia kwa njia ya kisasa, huduma ya kuweka nyonga na magoti bandia pamoja na huduma mionzi tiba kwa wagonjwa wa ngozi.
Hayo yamebainishwa mapema leo, akiwasilisha taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Rachel Mhaville amesema lengo la kuanzisha kwa huduma hizo ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza rufaa za wagojwa kwenda kutibwa nje ya nchi kutafuta matibabu hayo.
Amesema hospitali ilifanikiwa kuanzisha matibabu ya kupunguza uzito kwa watu wenye uzito uliopitiliza kwa njia ya uwekaji puto katika mfuko wa chakula kwa kutumia endoskopia na wengine kupunguza ukubwa wa tumbo kupitia upasuaji wa matundu madogo ambapo hadi sasa wananchi 155 wamewekewa puto, 44 wamefanyiwa marekebisho ya puto kulingana uhitaji wao na 11 wametolewa puto.
Kuhusu kuanzishwa kwa huduma za kuweka magoti na nyonga bandia, Dkt. Mhaville amesema katika kampasi ya Mloganzila wagonjwa waliopata maradhi ya viungo vya magoti ni 207 na nyonga 59 waliweza kupata huduma mpya zilizoanzishwa katika kampasi hiyo. Adha wagonjwa 10 wamefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa marejeo wa magoti na nyonga bandia.
0 Comments