Header Ads Widget

MMASUTA WAMUOMBA RAIS DKT SAMIA KUWASOPITI

Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp.

MTANDAO wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni Tanzania (MMASUTA) kupitia kikundi chake cha Sanaa za Maigizo kinachoitwa ‘Kazi Iendelee na Mama Samia’wameiomba Serikali kuwashika mkono wasanii chipuki kuwaalika kwenye matamasha na matukio Makubwa ya Kiserikali ili waweze kukuza vipaji vyao.

Aidha, shughuli zote za wameomba pia kupewa nafasi za kichama kupitia sanaa waweze  kunadi miradi ambayo imetekelezwa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Dkt David Msuya ambaye ni Mwenyekiti wa MMASUTA, mtandao huo una wanachama wenye vipaji vikubwa lakini hawajabahatika kuonesha uwezo wao kwenye matamasha makubwa.

Amesema kuwa, wao tayari kujitoa kwa ajili ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi kwani Rais aliepo madarakani amefanya mambo makubwa  ambayo wao wanahitaji kuyasemea na kuyatangaza kwa wananchi.

"Kuna mambo makubwa na mazuri ambayo yamefanywa na Rais Dkt Samia ikiwemo ujenzi wa SGR, shule, hospital, Ajira kwa vijana, mikopo ya asilimia 10, na mambo mengine mengi, haya yote tunahitaji kuyatangaza"amesema

Ameongeza kuwa, waliokutana leo ni wachache kati ya kundi kubwa ambalo lipo nyuma yao kilio chao kikubwa ni kumuomba Rais Dkt Samia awaone na wao kama wasanii chipukizi ili waweze kuendeleza vipaji hivyo.

"Hapa tumekutana wasanii mbalimbali ikiwemo wachongaji vinyago, wanamziki wa bongo fleva, waimbaji wa kwaya, bongo movie, waimbaji wa utenzi, wasomaji wa ngonjera na wengine kibao"

Ameongeza "Mara kadhaa tunapopata nafasi tunafanya shughuli mbalimbali za kuiunga mkono Serikali ikiwemo kufanya usafi katika Zahanati ambazo ni sehemu ya miundombinu ya afya ambayo imejengwa na Serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia, na kutokana na kuwa uzoefu huo tunamuomba Mama yetu atushike mkono nasi tuwe sehemu ya kutangaza miradi ambayo imetekelezwa chini ya uongozi wake, amesema kupitia sanaa yetu ya uigizaji, mashauri,nyimbo" amesema Dkt David

Dkt Msuya amesema wakati wa mafuriko aliweza kushiriki wilayani Kilosa mkoani Morogoro yakiwa yametokea  nao walikuwa sehemu waliofika kwa ajili ya kusaidia shughuli kadhaa za kibinadamu, hivyo wananaamini ikiwa watapatiwa nafasi ya kujumuika katika mikutano ya kiserikali na kichama wataweza kunadi vema mafanikio ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

"Wasanii mnaowaona hapa leo wana vipaji vya aina tofauti ikiwemo vile uchezaji wa ngoma za asili, uigizaji, utunzi wa mashairi, ngonjera na uigizaji wa maigizo hivyo tukishirikishwa ipasavyo katika kazi mbalimbali za Serikali tutaweza kuzitangaza vyema kupitia vipaji wasanii hawa," amesema Msuya.

Hata hivyo Wasanii hao chipukizi wamekaa na kutafakari na kuamua kumuomba Rais Samia awaweke katika timu ya itakayoshriki katika majukwaa yote ya kiserikali na kichama kwa pamoja kutangaza kazi ambazo zimetekelezwa na ili wananchi waweze kuzielewa kwa kina.

Zainabu Jaha ambaye ni Katibu Msaidizi amesema ikiwa watapewa nafasi hiyo watafanya vitu tofauti kupitia uigizaji, ngonjera ambazo zinazoeleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, (SGR).

Pia ujenzi wa Zahanati nchi nzima ambazo kwa njia moja au nyingine zimepunguza vifo vya mama wajawazito na kuweka salama maisha ya kundi hilo wakati wa kujifungua na ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI