Header Ads Widget

MEZA YA MAGAZETI IJUMAA MACHI 14/2025:MWENYEKITI WAZAZI CCM AUAWA KIKATILI ,BENKI YA DUNIA YAMPA KONGOLE RAIS SAMIA ,MBUNGE KABATI ASIFU JITIHADA ZA FOXE'S KUSAIDIA WENYE ULEMAVU MUFINDI..

 

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM AUWAWA KIKATILI. 

 Na Moses Ng'wat, Songwe. 

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chitete wilayani Ileje, Halisoni Mwampashi (62), ameuawa kikatili na watu wasiojulikana. 

 Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Joseph Mwashitete, tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Ntembo, usiku wa Machi 12, 2025, majira ya saa tatu usiku wakati marehemu akirejea nyumbani kutoka kwenye vilabu vya pombe maarufu kama Gezaulole. 

 Mwashitete alisema alipokea taarifa za mauaji hayo kutoka kwa Waisoni Sikaumba, ambaye baadaye alifika eneo la tukio na kuwakuta watu wakiwa wamekusanyika, wakiwemo wake wa marehemu na mtoto wake wa kiume, Jose Mwampashi ambapo mwili wa marehemu ulikuwa umetelekezwa barabarani.

 "Nilipofika eneo la tukio nilikuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha kichwani na nilitoa taarifa Kituo cha Polisi Itumba, ambao walifika haraka na kuuchukua mwili kwa ajili ya uchunguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje," alisema Mwashitete. 

 Hadi sasa, chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, lakini wananchi wa kijiji hicho wameahidi kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Marehemu azikwa, CCM watoa neno. 

 Katika mazishi yaliyofanyika Machi 13, 2025, Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Chitete, Daima Silwamba, alisema chama hicho kimepata pigo kubwa, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kwani marehemu alikuwa kiongozi muhimu. 

 "Tunaomba vyombo vya dola vifanye uchunguzi wa kina na kuhakikisha haki inatendeka. Tunapaswa kushirikiana na polisi ili wahalifu wafikishwe mbele ya sheria," alisema Silwamba. 

 Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ileje, Maoni Mbuba, aliwataka wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutafuta suluhu kupitia viongozi wa serikali na jamii. 

 Mtoto wa marehemu, Jose Mwampashi, alieleza masikitiko yake kuhusu kifo cha baba yake, akisema hakutarajia kukuta mwili wake ukiwa barabarani alipokuwa akienda kula chakula cha usiku.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema bado hajapokea taarifa rasmi lakini ataifuatilia na kutoa taarifa kwa umma mara uchunguzi utakapokamilika. 

 Mwili wa marehemu umepumzishwa katika makaburi ya kijiji cha Ntembo huku familia, ndugu, jamaa na wanachama wa CCM wakiendelea kuomboleza msiba huo mzito. Mwisho.
Mbinu rahisi ya kupata mkopo wa fedha nyingi 

 Kwa miaka wafanyabiashara wengi wa ndani na wale kimataifa wamekuwa wakiangaika kusaka mikopo yenye masharti na riba nafuhu ili kukuza biashara na miradi yao ya kiuchumi. 

 Mimi nilikuwa mmoja wao ambaye nilisumbuka sana kutafuta mkopo ambao utawezesha kukamilisha mradi wangu wa umeme jua ambao nililenga kuzalisha umeme mwingi kwa ajili ya kuuza kwa wakazi wa eneo langu. 

 Kila taasisi ya kifedha ambayo nilipeleka wazo langu la kibiashara walikuwa wanasema inaonekana litachukua muda mrefu na isitoshe hakuna uhakika kama kweli litafanikiwa. 

 Baada ya kuona hivyo, ndipo nikaenda kwa Kiwanga Doctors huko Migori nchini Kenya na kueleza shida yangu. 

Nashukuru aliweza kunielewa na kunifanyia kile kinachojulikana kama quick loan approval spell. 

 Haikuchukua muda nikapigiwa simu na moja ya kampuni ambazo hapo awali niliwahi kutuma maomba ya mkopo kwao. Waliniambia mkopo wangu upo tayari hivyo nifike kwa ajili ya kuupata. 

 Mara moja nilifika katika ofisi zao na kupatiwa mkopo wangu, nilianza kufanya mradi wangu hadi sasa umekuwa mkubwa ambapo nazalisha umeme jua pia nauza sola paneli katika maeneo mbalimbali nchini. 

 Kwa sasa taasisi ile inaweza kunikopesha hadi kiasi cha Sh1.2 bilioni kutokana kampuni yangu imekuwa kubwa sana ikitoa ajira kwa mamia ya watu katika vitengo mbalimbali. 

 Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio ya kibiashara kutokana huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116 469840 au tembelea tovuti yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI