Header Ads Widget

MEZA YA MAGAZETI ALHAMISI MACHI 12/2025:TRA YA VUNJA REKODI YA MAKUSANYO,MWENYEKITI UWT MUFINDI AIPA KONGOLE CCM KWA KUWEKA UKOMO WA VITI MAALUMU,TULI MAKONGO: MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU


 

>
MZAZI WA MTOTO MWENYE ULEMAVU ALIYESAIDIWA KUANZA KUJITEGEMEA ATOA PONGEZI
Na Berdina Majinge Matukio Daima Media, Mufindi 

 Wananchi wameshauriwa kuacha tabia mbaya ya kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu badala yake wawatoe ili waweze kupata elimu na misaada ya kijamii yakiwemo Mafunzo ili kuepuka kuwa tegemezi.

 Ushauri huo umetolewa Jana na Tuli Makongo mzazi wa Hermani Kangalawe ambaye ni mlemavu aliyenufaika na Mafunzo yanayotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Foxes Community and Wild Life Conservation na Mradi wa Youth Angency Mufindi (YAM) chini ya Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

 Kuwa Mradi wa YAM ni Mradi ulioanza mwaka 2021 kwa kufanya kazi miaka minne hadi mwaka 2024 Mradi huu umefadhiliwa na serikali ya Filands chini ya taasisi yake ya Diaconess kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation Tuli mbali ya kushukuru Mradi wa YAM na Taasisi ya Foxes kwa kumchukua mtoto wake kwa ajili ya mafunzo mbalimbali ambapo kwa sasa amejifunza fani ya kuchonga na anawasaidia wazazi wake kwa shughuli kadhaa za nyumbani alisema mtoto wake amekuwa msaada mkubwa. 

 "Kwa sasa Hali yake inaendelea vizuri tangu ajiunge na mradi wa YAM anafanya kazi vizuri amejifunza kuchonga ameshatuletea bidhaa anazozichonga kwa kweli tunawashukuru walimu wanaowafundisha pamoja na Foxes "alisema 

Kabla ya mradi huo alikuwa ni mtu wa kushinda nyumbani hana pa kwenda na hawezi kulima wala kufanya kazi yeyote,lakini tangu walivyomchukua anaendelea vizuri anavyofanya kazi anakuwa na ushirikiano na mzazi pamoja na walimu ambapo anapata mafunzo hayo

 Alisema kuwa anaishukuru kampuni ya Foxes kwa kuwasaidia na amejiandaa baada ya mafunzo hayo kumuendeleza na fani aliyochagua ili iweze kumsaidia katika kujiingizia kipato na kuwasaidia wazazi.

 "Wazazi wasiwafiche watoto majumbani wawatoe wawapeleke kwenye vituo wapate huduma mbalimbali ili waweze kujifunza na kuanza kujitegemea kipato na kutusaidia wazazi". 

 Aliomba serikali iendelee kuwachukua watoto mitaani na waliofichwa majumbani na wazazi wanaowaficha watoto hao sio vizuri kwa sababu mtoto akikaa nyumbani anazidi kuwa mlemavu hawezi kuelewa chochote wala kufanya fani yeyote. 

 "Serikali ikimchukua mlemavu huyu atapata msaada mbalimbali ikiwemo mafunzo ya ujasiliamali na kujitegemea anakuwa na uelewa na anakuwa msaada kwa wazazi pia pale alipo anapata pesa na anatusaidia hata sisi wazazi"

Kuwa kwa sasa amekuwa msaada mkubwa anafanya kazi mbalimbali kama kupasua kuni, kuchota maji, kufua nguo hii inanisaidia mimi mzazi

 Hermani kangalawe ni kijana mwenye ulemavu na mradi wa YAM kwa sasa unashughulika na vijana 134 wenye ulemavu. 

 MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI