NA HAMIDA RAMADHAN,MATUKIO DAIMA SINGIDA
MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, amekabidhi pikipiki sita kwa UVCCM Mkoa wa Singida, ambazo zitawafaidisha makatibu wa wilaya zote sita za mkoa huo.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa RC Mission Mkoani Singida, Mbunge Kingu pia amepeleka bati 120 zenye thamani ya milioni 3.1 kwa UWT, tiles zenye thamani ya milioni 7 kwa ofisi ya CCM Wilaya ya Ikungi, pamoja na shilingi milioni 3 kwa jumuiya za Wilaya ya Ikungi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida, ambaye alishuhudia uzinduzi wa miradi ya kiuchumi ya UVCCM, ikiwemo vibanda vya biashara 73 na kampasi ya elimu ya kati ya Chuo St. Joseph.
Kingu alisisitiza dhamira yake ya kuwasaidia vijana na kutoa risiti ya ununuzi wa pikipiki hizo, akisema alitumia jumla ya milioni 16.2. Pikipiki hizo zimeandikishwa kwa jina la UVCCM na hazidaiwi kodi yoyote.
Mwisho
0 Comments