Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amechangia mifuko 250 ya saruji kwenye ujenzi wa shule ya sekondari Nyabakangara.
Harambee hiyo iliyofanyika machi 25,2025 kwenye Kitongoji cha cha Kamatondo Kata ya Nyambono ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo wa CCM,wazawa wa Kata hiyo na wadau wa maendeleo wakiwemo wa elimu.
Akizungumza kwenye harambee hiyo mbunge Muhongo amesema elimu bado ni kipaumbele ndani ya jimbo na ndiyo inayopelekea jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule.
Amesema ili kumsaidia mwananchi wa Musoma Vijijini ni pamoja na kumpa elimu mtoto wake kwa manufaa ya baadae.
Mbunge Muhongo amesema kila mmoja anakaribishwa kwenye jimbo la Musoma vijijini kuchangia maendeleo ya elimu ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
"Ndugu zangu kipaumbele chetu namba moja bado ni elimu na ndio maana tunafanya jitihada mbalimbali zikiwa ni pamoja na kuendesha harambee za ujenzi wa shule na kuandaa mijadala ya kuinua kiwango cha ufaulu kwenye shule zetu.
" Leo ntachangia mifuko 250 ya saruji katika ujenzi wa shule ya Nyabakangara lakini awali kupitia mfuko wa jimbo imeshatolewa mifuko 150 kwenye ujenzi huu",amesema.
Licha ya uchangiaji huo wa mbunge wa jimbo mifuko ya saruji 204 ilichangiwa na wanakijiji na wadau mbalimbali,tripu 5 za mawe na fedha taslimu kiasi cha shilingi 448,000 na tayari matofali 3,700 yamefyatuliwa.
Kamati ya Ujenzi Iliundwa jana kwa kila Kitongoji kutoa mjumbe mmoja na kamati kuwa na wajumbe saba (7)
Uamuzi wa Wanakijijiujenzi uanze mara moja na halmashauri iharakishe upatikanaji wa ramani za ujenzi
Leo machi 26 mbunge wa Jimbo anapiga harambee ya ujenzi wa Kataryo sekondari ya Kijiji cha Kataryo Kata ya Tegeruka ambapo Kata ya Nyambono na Tegeruka wanaanza ujenzi wa shule ya pili kwenye Kata zao.
0 Comments