Na. Kwiyeya Singu.
Ndugu Peter A. Mashili, ambaye pia ni Mwenyekiti wa wachimbaji wa dhahabu, amempongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hasan ktk miaka yake minne madarakani.
Akiongea na waandishi wa habari Wilayani Nzega, Mashili alisema, "Tunamshukuru sana Mama yetu mpendwa, Rais Dk Samia Suluhu Hasan katika miaka yake minne (4) ya uongozi wake; ameboresha sana sekta ya madini.
Huko nyuma hatukuwa na uwezo mkubwa lakini sasa tumeweza kuwa na uwezo mzuri kutokana na fursa tulizopewa na Rais wetu mpendwa.
Hiki ni kiwanda cha kuchenjulia dhahabu ambacho nimekijenga ndani ya miaka minne ya Rais Samia na kimeturahisishia sana kazi zetu, zamani tulikuwa tunahangaika kwenda mbali, lakini sasa tunamaeneo yetu ya kuchenjulia wa dhahabu.
Kiwanda hichi kipo Wilaya ya Nzega na kimewarahisishia sana wachimbaji wadogowadogo ndani na nje ya Nzega kwani wanakuja hapa kupembua dhahabu hapa karibu na kwa wakati, na wanapata haki zao bila shida yo yote.
Lakini pia, katika miaka hii minne, Rais Dk. Samia amedhibiti mapato, utoroshaji wa dhahabu hakuna tena, kwa sasa huwezi kuyeyusha dhahabu pasipo na mamlaka ya serikali, ni lazima awepo OCD (Mkuu wa Polisi), DC (Mkuu wa Wilaya), Usalama wa taifa, Afsa Madini ili waweze kukata mapato na kuruhusu hatua zingine za mwisho kama kulipa kodi TRA ziendelee.
Mashili
Ombi letu kwa Mama Samia, Rais wetu aendelee kufanya kazi na kuwatumia wataalamu wake kote nchini kuhakikisha vijana wengine wanaojishughulisha, na wale wanaotaka kuchimba madini wapewe fursa ili kuongeza uchumi ktk taifa letu. " Peter Mashili.
Safi sana. Lakini pia nitumie nafasi hii kuwapongeza waandishi wa habari kwa kufuatilia utekelezaji wa sera hizi za umma, kwani hii inasaidia sana kuleta maendeleo ndani ya jamii.
Sera nyingi za kisekta zinakabiliwa na changamoto nyingi ktk utekelezaji kama hakuna wandishi wanaofuatilia utekelezaji wa sera hizi itazuia maendeleo.
Kutokana na hilo, ni vyema waandishi wa habari kuelewa sera na namna ya kuzichambua sera mbalimbali za umma na kutoa taarifa kwa jamii au mapendekezo kwa watunga sera hizo ili kuzifanyia marekebisho pale ambapo sera hizo zinapitwa na wakati au kuwaumiza wananchi ambao ndio wadau na washiriki wa moja kwa moja wa maendeleo.
Kazi kuu ya waandishi wa habari ni kuiunganisha jamii na watekelezaji wa sera hizo ktk kutoa nafasi ya uamuzi wa umma ili kuleta ushirikishwaji ktk utekelezaji.
Hilo haliwezi kutokea kama waandishi wa habari hawazielewi sera za umma, ni muhimu kuzielewa sera ili kuongeza uwajibikaji miongoni mwa watekelezaji.
Lakini pia, nimpongeze Mwenyekiti wa wachimbaji madini, ndugu Peter A. Mashili kwa kusimamia haki na wajibu wa wachimbaji wadogowadogo wa madini ktk kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Kiongozi mwenye maono ni kionyesha njia kwa wale anaowaongoza, na huyatangulia mapambano, huwaunganisha watu wake na mamlaka nyingine pia.
Na mwisho kiongozi huwatanguliza wengine wakati wa mafanikio.🤝
0 Comments