NA CHAUSIKU SAID MATUKIO DAIMA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Mwanza wametembelea kituo Cha hisani na yatima Islamic Foundation vya kulelea watoto yatima pamoja na wenye mahitaji maalum vilivyopo Wilaya ya Ilemela na kutoa msaada lengo likiwa kurudisha fadhira Kwa jamii kutokana na shughuli wanazozifanya na mafanikio wanayoyapata katika ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo meneja wa TRA Faustine Cosmas ameeleza kuwa wameamua kutoa msaada huo ili watoto hao waweze kuahiriki mafanikio wanayoyapata katika kusherekea sikuuu ya edd el fitri baada ya kumaliza mfungo na pasaka baada ya kumaliza kwarezima.
Faustine amesema kuwa Mamlaka hiyo inajali walipa kodi wake na wameamua kuwashika mkono watoto hao kwa kutoa mahitaji mbalimbali vikiwemo vyakula, mashuka, vyandarua,pamoja na nguo za kujistili watoto wa kike ili na wao waendelee kufurahi katika vituo hivyo.
"Tumeamua kutembelea vituo viwili vya watoto yatima na wenye mahitaji maalum Kwa kuwaletea mahitaji waliokuwa wameelezea Kwa ajili ya maandalizi ya sikuuu hizi mbili ya edd el fitri na pasaka"Alisema Faustne.
Walezi wa vituo hivyo Abdallah Omary Mkuu msaidizi kituo ChaYatima Foundation na Grace peter Meneja kutoka kituo cha Hisani wakizungumza kwa nyakati fouti wamesema kuwa vituo vya kulele watoto wenye mahitaji maalum vinamahitaji mengi na wanawaomba wadau, mashirika na tasisi mbalimbali zilizopo Jiji hapa kujitoa kuwasaidia watoto hao ili waweze kukidhi mahitaji Yao wawpo katika vituo hivyo.
Kwa upande wao watoto wa vituo vyote viwili wameishukru Mamlaka ya mapato Tanzania Mkoa wa Mwanza Kwa kuwakumbuka na kuwapatia mahitaji maalumu hususani katika kipindi hiki Cha sikukuu ya edd el fitri pamoja na pasaka.
" Tunawashukru sana TRA Kwa kutukumbuka tunawaombea Kwa Mungu pale walipotoa wasiweze kupungukiwa wakazidi kubalikiwa katika kazi zao wanazofanya Kila siku" Alisema.
0 Comments