Header Ads Widget

MAMA LULIDA AKUTANA NA MAKUNDI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU KUPATA FUTARI YA PAMOJA

NA HADIJA OMARY....

Mbunge wa kuteuliwa  mkoani Lindi Riziki Lulida ameungana na watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo walemavu wazee na mayatima wa Mkoa huo katika kupata futari ya pamoja.

Tukio hilo limefanyika Katika  viwanja vya Ilulu  huko Manispaa ya Lindi  ambapo pamoja na makundi hayo maalumu pia waumini wengine wa dini ya kiislamu waliweza kupata futari  hiyo

Sambamba na futari hiyo  ilihusisha pia  zoezi la kutoa msaada wa viti mwendo vitatu  kwa  wenye uhitaji chini ya ufadhiri wa  Taasisi ya Riziki Lulida foundation 

Akizungumza baada ya ifari hiyo shekhe Mkuu wa Mkoa huo Mohamedi Mushangani aliwasihi waislamu kuendelea kufanya ibada ya funga kwani ni moja kati ya nguzo tano za uislamu kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha quran tukufu. 

Alisema muislamu yeyote ambae amejaaliwa uzima na kwamba hana tatizo lolote la kiafya anapaswa kuitekeleza nguzo hiyo muhimu ya uislamu Kwani saumu ni mkombozi kwa waislamu hivyo ikifika mwezi wa ramadhani inapaswa wafunge kweli kweli ikiwa pamoja na kufanya mambo mema na mazuri.

“zipo hadithi zilizotelemshwa kwa mitume na maswahaba wetu zikieleza yeyote atakaefunga ramadhani hali ya kuamini kulipwa heri na kutaraji kupata thawabu basi huyo mungu atamsamehe makosa yake yote aliyoyatanguliza lakini mwenye kula mchana wa siku moja tu ya ramadhani pasipo na sababu yoyote iliyomfanya ale mchana mtu huyo hawezi kulipa saumu yoyote ya kuilipisha siku ile aliyofungua pasipo sababu hata kama atafunga mwaka mzima” Shekhe Mushangan

Mbunge wa kuteuliwa Riziki Lulida na mkurugenzi wa lulida foundation aliwashukuru wananchi waliojitokeza kujumuika nae kwenye tukio hilo muhimu   kwani kufanikiwa kwa ghafla hiyo kumetokana na ujio wao

Alisema ameamua kukutana na Watu HAO wenye mahitaji maalumu kupatanao iftari hiyo Lengo lake kubwa pia ni kufanya Dua ya pamoja kwa ajili ya kumuona Rais Samia suluhu Hassan kwa mwenyezimungu amjaalie Afya njema ili aendelee kuwahudumia watanzania 

Amesema kupitia Taasisi yake aliyoianzisha ya Riziki Lulida foundation amedhamilia kuwasaidia Watu wenye mahitaji maalumu Katika mahitaji mbalimbali ikiwemo viti mwendo, mafuta , sababu na visaidizi vinginevyo 

Akitoa salamu za Serikali Katibu tawala Wilaya ya Lindi Hudhaifa  Rashid aliwasihi waislam na  kuyaisha Yale mema yote wanayoyafanya wakati huu wa Mwezi mtukufu wa ramadhani huku shekhe Mkuu wa Wilaya hiyo Ismail Mnape akimpongeza Mbunge huyo kwa kuwakumbuka Watu wenye mahitaji maalumu 



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI