NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMA.
KAMPUNI ya Kilimanjaro One Sports Promotion Limited inatarajia kuanzisha mbio za kiutalii Jijini Mwanza juni 27 Hadi 29 lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya kiutalii na fursa za kiuwekezaji zinazopatikana katika kuelekea katika tamasha la kiutamaduni la Kanda ya ziwa litakalodanyika Mkoani Simiyu
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Sports Promotion Limited, Mohamed Khatibu wakati alipokuwa akizungunza na na waandishi wa habari, wadau wa utalii pamoja na baadhi ya wanariadha jijini hapa.
Alisema utalii wa mbio hizo utajumuisha watoto, wanafunzi, walemavu, wamama wajawazito,makundi mbalimbali ya mazoezi, viongozi wa daraja la kwanza ndani ya mkoa na kanda ya ziwa kwaujumla pamoja na wananchi wote.
"Madhumuni makubwa ya mbio hizi ni kutangaza vivutio vya kiutalii na fursa za kiuwekezaji zinazopatikana katika Jiji la mwanza ili kukuza uchumi wa kanda ya ziwa na Taifa kwaujumla", Alisema Khatibu
Aidha, alieleza kuwa kila uwekezaji wa kiuchumi unahitaji utulivu wa nchi na amani ya watu wake, hivyo watatumia mbio hizo kuhamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha na kushiriki uchanguzi Mkuu Oktoba 2025 kwa amani.
Alisema wanakusudia kuwa na zaidi ya watu 2,000 katika tukio hilo na zawadi nzuri kwakila kundi zimeandaliwa wakati wa kuzindua rasmi zitatangazwa ili kuwavutia watu wengi zaidi kushiri.
Kwaupande wake Msimamizi Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Rhoda Kabarua alisema watatumia michezo kama mkakati wa kutangaza utalii nchini kutokana na michezo kuwa uchumi,afya na utalii.
"Michezo inaleta watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo mkoa utapata ongezeko la uchumi,watu watafanya mazoezi afya zitaimarika na watapata fursa ya kutembelea vivutio na mazao ya utalii",
Naye Mtaribu wa Huduma ya Afya ya Uzazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana, alisema mbio hizo ni fursa kubwa kwani itawasaidia kuendelea kutoa elimu kwa wajawazito ambayo itasaidia kupunguza vifo.
Alisema katika mbio hizo wajawazito watashiriki kwakufanya mazoezi mepesi ikiwemo kutembea kwa dakika 20 hadi nusu saa hatua itakayosaidia kuimarisha afya zao.
"Kunafaida nyingi za kufanya mazoezi kwa wajawazito,ikiwemo kupunguza uzito,kusaidia mzunguko wa damu kwenda vizuri pamoja na kupata usingizi mzuri", Alisema Yohana
Pia aliongeza kuwa kwa mama mjamzito mwenye upungufu wa damu,mwenye historia ya mimba kuharibika hataruhusiwa kufanya mazoezi hayo.
Amani Issa ni mtoto atakaye shiriki mbio ya kiutalii amewaomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki mbio hizo ili waweze kuimarisha afya zao.
Mwisho.
0 Comments