Header Ads Widget

KIJANA MWENYE ULEMAVU ALIYEUNGUA MOTO WAKATI AKIANDAA SHAMBA ASAIDIWA NA TAASISI YA FOXES

 

Na Matukio Daima Media 

KIJANA mwenye Ulemavu Mkazi wa kijiji cha Ikanga kata ya Mdabulo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Yusto Kalinga ambae Ulemavu wako ulitokana na kuungua moto Mwili mzima wakati akiandaa shamba kwa kuchoma nyasi amekuwa miongoni mwa Vijana wenye Ulemavu 134 wanaopatiwa  Mafunzo ya ujasiriamali kupitia Taasisi ya taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation  na Mradi Youth Agency Mufindi (YAM).

Kijana huyo amepongeza Mradi huo wa YAM chini ya Taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kwa kumuona na kumpatia fursa hiyo ya Mafunzo .

 Akizungumza Jana wakati wa Mafunzo ya Siku 12 yanayoendelea ukumbi wa Yatima Igoda Mufindi kwa Vijana hao wenye Ulemavu 134 Kijana huyo alisema kuwa Mafunzo hayo yanaelekea kumpa kipato na kuondoka na Vijana tegemezi kwa familia.

Yusto alisema kuwa malengo yake ni kuwa mfugaji mkubwa wa kuku kwa sababu kutokana na ulemavu alionao anaweza kuzifanya shughuli hizo kwa mikono yake mwenyewe na kumuingizia kipato.

Yusto ni mmoja wa walemavu 134 ambao wanapata mafunzo kupitia taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation na mradi wa Youth Agency Mufindi(YAM) kutoka vijiji 16 vya kata tatu za Wilaya ya Mufindi ambazo ni kata ya Mdabulo, Luhunga na Ihanu.

"Nimechagua kufuga kuku wa kienyeji na nina hitaji kujifunza zaidi kuhusu ufgugaji ili mafunzo yatakapomalizika nitakuwa nimejua nitajikita katika kufuga mifugo gani zaidi"

Akizungumzia jinsi alivyopata ulemavu huo alisema kuwa siku moja ambayo hatoisahau katika maisha yake walikuwa wameenda kuchoma shamba na mwenzake  ambaye walikuwa wakifanyakazi pamoja kwa muda mrefu walizingirwa na moto na moshi kumzidi na kujikuta kadondoka na kuungua mikono.

"Wakati tunasafisha shamba kwa kutumia moto kwa bahati mbaya moto ukatoka tulijitahidi kuuzuia lakini moshi ulituzidi na kutuzingira na kudondoka nakaungua mikono yote miwili,nimekuwa nikijiuguza kwa muda mrefu huku nikipambana kwa hali na mali ili nisiwe na ulemavu wa kudumu"

"Nawashukuru taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation  kwa kunisaidia kupata matibabu kutoka katika hospitali Inuka mkoani Njombe pia  kufanya mazoezi ili mwisho wa siku mikono yangu iwe vizuri, nawashukuru wao kama taasisi kwa kutuwezesha kupata mafunzo na kuwekeza katika ulemavu wetu na kutufanya tuweze kujitegemee"alisema

Aliwashauri washiriki wa Mafunzo hayo  ambao wanapata mafunzo katika mradi huo kusikiliza ushauri wa mkufunzi na kuwatumia katika maisha yao ya kila siku kuhakikisha yale yaliyojifunza yanaleta mafanikio katika maisha yao. 

Mradi   YAM Mradi ulioanza mwaka 2021 Hadi 2024 kwa kufanya kazi miaka minne  kusaidia Mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha Vijana wenye mazingira magumu kutoka kata tatu za Ihanu,Mdabulo na Luhunga Mradi huu  umefadhiliwa na    serikali  ya Filands  chini ya taasisi yake ya Diaconess   kwa  ushirikiano  wa  serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya  wilaya  ya Mufindi na taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI