NA BERDINA MAJINGE, MATUKIO DAIMA MEDIA
Kesi ya mauaji ya aliyekuwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Christina Kibiki imeahirishwa hadi machi 24 mwaka huu kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo amesema kuwa kesi hiyo utakuja March 24 katika mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa kutokana na upande wa jamuhuri kutokukamilisha upelelezi wake.
kwa upande wa Mawakili wa Jamhuri Radhia Njovu na Cecilia Mrisho uliiiomba mahakama kuahirisha kwa kesi hiyo kutokana na kuendelea na upelelezi ambao bado haujakamilika.
Upande wa utetezi unaowakilishwa na Barnabas Nyalusi, kutoka kampuni ya Mawakili ya BLS Attorney &Partner ameiomba Mahakama kuhimiza upande wa jamuhuri kukamilisha upelelezi kwa wakati ili kesi hiyo ianze kusiskilizwa.
Waliofikishwa Mahakamani hapo ni pamoja Boniphace Yohana Ugwale ambae ni diwani wa kata ya Nyanzwa Kilolo Kefa John Wales,Silla Johnson Kimwaga,Boniphace Yohana Ugwale ,Willy Gerald Chikweo na Hedikosi Gwerino Kimwaga kwa pamoja wanashitakiwa kumuua Christina Kibiki.
Washitakiwa hao walitenda kosa hilo la mauaji Novemba 12 mwaka 2024 katika Kijiji Cha Ugwachanya wilaya ya Iringa Vijijini.
Washitakiwa wamerudishwa rumade hadi machi 24 mwaka huu itakapoletwa kwaajili ya kutajwa tena.
mwisho.
0 Comments