Header Ads Widget

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA KUZINDULIWA KESHO ARUSHA

 


 Na Elizabeth Zaya Habari na Matukio App 

MKUU wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameiomba timu ya Wanasheria wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, kuorodhesha majina ya watumishi wa serikali wanaolalamikiwa na wananchi kusababisha migogoro inayochochea wakose imani na serikali.


Makonda ametoa kauli hiyo leo alipokutana na wataalamu wa sheria, mawakili na maoofisa maendeleo ya jamii pamoja na wakuu wa idara mbalimbali kujadili mikakati ya kutatua changamoto za wananchi katika halmashauri saba za mkoa wa mkoa huo.


Amesema baadhi ya watumishi wakiwamo maofisa wa maendeleo ya jamii, wamekuwa wakipindisha sheria kwa maslahi yao binafsi, hivyo akaiomba timu ya Kampeni hiyo ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kuandika majina yao na kuwasilisha ripoti baada ya kumalizika kwa kampeni hiyo.


Kampeni hiyo ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, inazinduliwa kesho katika mkoa wa Arusha na baada ya hapo itafikishwa katika halmashauri zote za mkoa huo.


“Kuna watunmishi wanatajwa kwa kukwamisha haki za wananchi, tunataka majina yao, na timu hiii ianishe changamoto zote zilizoibuliwa ili mashirika na idara husika kama Jeshi la Polisi, Uhamiaji na idara ya kazi zichukue hatua stahiki,”amesema Makonda.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ester Msambazi, amesema Arusha utakuwa ni mkoa wa 23 kufikiwa na kampeni hiyo tangu izinduliwe rasmi mwaka 2023.

Kwa mujibu wa Msambazi, uzinduzi wa kampeni hiyo katika mkoa wa Arusha kesho, utafanywa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro na kuwataka wananchi kwenda kupata msaada wa kisheria bure kutoka katika taasisi na idara mbalimbali za serikali katika viwanja vya Ngarenaro.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI