Na Fadhili Abdallah,Kigoma
TIMU ya soka ya Kajuna FC ya mkoani Kigoma imezidi kujiimarisha katika mashindano ya mabingwa wa mikoa kundi B kituo cha Kigoma baada ya kuendelea kupata ushindi wa tatu mfululizo wa mashindao hayo yanayofanyikwa kwenye uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Kajuna imepata ushindi huo baada ya kuichapata timu ya Magic Pressure ya Singida kwa magoli 2-1 hivyo kufikisha pointi tisa na kuongoza kundi kundi hilo lenye jumla ya timu saba.
Katika mchezo huo magoli yote ya timu ya Kajuna yalifungwa na Ally Sonso katika kipindi cha pili cha mchezo sambamba na goli la Magic Pressure ambalo pia lilipatikana kipindi cha pili likifungwa na Ramadhan Ramadhan katika mchezo uliochezeshwa na Mwamuzi Ndaki Mussa kutoka Tanga.
Timu hiyo ya mkoa Kigoma imeshacheza michezo mitatu kati ya michezo sita ambayo kila timu inapaswa kucheza kwenye kundi hilo matokeo ambayo yanaipata nafasi ya kuwa moja ya timu mbili zitakazotoka kituo hicho kwa ajili ya kucheza hatua ya robo fainali.
Wakati timu ya Kajuna ikiongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi tisa kwa sasa inafuatiwa na timu ya Home Boys ya Katavi yenye point saba huku timu ya Igunga kutoka mkoani Tabora ikiwa na Point nne na timu ya Kyela ya Mbeya ikiwa na point tatu.
0 Comments